January 6, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dk Mwinyi ameifungua Skuli Kisiwani Tumbatu yagharimu Sh. Bii 7

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

RAISI wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi ameifungua Skuli ya Kwanza ya Ghorofa Kisiwani Tumbatu iliyogharimu Shillingi Bilioni
7.015.

Akizungumza na Wananchi baada ya kuifungua Skuli hiyo Rais Dk, Mwinyi ameziagiza Mamlaka zinazoshughulika na ajira kuhakikisha zinatoa fursa za ajira kwa Vijana wa Tumbatu wenye sifa zinazohitajika.

Dk,Mwinyi ametoa tamko hilo alipoifungua skuli ya Sekondari ya Tumbatu ,Wilaya ndogo Tumbatu Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Rais Dk, Mwinyi amezitaka Mamlaka hizo katika Sekta za Afya,Elimu , Miundombinu, Maji , Umeme na nyenginezo kusimamia agizo hilo ili miradi iliyomo Tumbatu ilete tìja kwa Wananchi na kuongeza Ufanisi.

Aidha Rais Dk,Mwinyi ameeleza kuwa Serikali inakusudia kujenga Nyumba za Walimu na Dakhalia ili Walimu watakaofundisha katika Skuli ya Tumbatu waishi katika Nyumba hizo.

Rais Dk, Mwinyi amewahakikishia Wananchi wa Tumbatu kuwa kinaçhofanyika sasa ni Utekelezaji wa Ahadi zake na kwamba zitaendelea kutekelezwa zaidi .

Akizungumzia suala la Utalii ameeleza kuwa Serikali haina nia ya Kupeleka Shughuli za Utalii Kisiwani humo na kuwataka wananchi kuyaepuka Maneno yasio na Ukweli yanayoenezwa na Watu wasiopenda Maendeleo.

” Sina nia ya kuleta UtaliiTumbabu,Utalii utapelekwa kwa Watu wanaoutaka sio Tumbatu” alisisitiza Dk,Mwinyi.

Rais Dk, Mwinyi amewahimiza Vijana Kusoma kwa bidii kwa lengo la kuongeza Ufaulu kufuatia kuwepo kwa Skuli yenye Viwango vya Ubora ,Maktaba, Maabara ya Kisasa ya Sayansi na Madarasa mazuri.

Rais Dk,Mwinyi akizungumzia Changamto zilizomo Kisiwani humo amefahamisha kuwa Serikali inaendelea na Ujenzi wa Hospitali Mpya ya Wilaya,Ujenzi wa Barabara ya lami ambayo Mkandarasi anaendelea na Ujenzi Pamoja na kutoa Agizo kwa Wizara ya Ujenzi Mawasilano na Uchukuzi kumpa Mkataba Mkandarasi ili kuendelea na Ujenzi wa Gati aliyoielezea kuwa na Umuhimu mkubwa kwa Kisiwa hicho hivi sasa.

Kuhusiana na suala la Maji ameiagiza Mamlaka ya Maji ZAWA kuchukua juhudi maalum kukamilisha Visima vya ziada ili kumaliza tatizo la Maji.

Aidha Dk,Mwinyi ameliagiza Shirika la Umeme kuondoa changamoto ya Kukatika kwa Umeme mara kwa mara tatizo alilolielezea kuwa ni la nchi nzima.

Rais Dk,Mwinyi ameipongeza Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kwa Usimamizi Mzuri wa Ujenzi wa Skuli Mpya Katika Maeneo mbalimbali hapa nchini.

” Hakika nimefurahi na nimeridhika na kazi nzuri mna yoifanya ” alisema Dk, Mwinyi

Naye Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Lela Muhammed Mussa amesema Lengo la Wizara ni kuanzisha Masomo ya Michepuo katika skuli hiyo ambayo itawaunganisha Wanafunzi wote wa Zanzibar .

Waziri Lela ameielezea miaka Minne ya Uongozi wa Dk, Mwinyi kuwa imewaondoshea Ujinga ,Maradhi na Umasikini Wananchi wa Zanzibar.

Akitoa Taarifa ya Kitaalamu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Khamis Abdalla Saidi amesema takribani Shilingi Bilioni 7.015 zimetumika kukamilisha Ujenzi huo wa Skuli ya Ghorofa tatu,Madarasa 41 yenye Uwezo wa kuchukua Wanafunzi 1,845 kwa Mkondo mmoja.