December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Diwani Mtoka awataka makatibu uwt kuongeza wanachama Kisukuru

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

DIWANI wa Viti Maalum Wanawake wilaya ya Ilala, Semeni Mtoka,amewataka makatibu wa umoja wanawake UWT kuongeza wanachama wapya wa Jumuiya hiyo kwa kushirikiana na wajumbe wa mashina na mabaraza ya UWT .

Diwani Semeni mtoka, ambaye ni Mlezi wa Umoja wanawake UWT Kata ya Kisukuru alisema hayo katika ziara yake ya kuangalia uhai wa Jumuiya pamoja na kuongea na makatibu wa matawi wa uwt na wajumbe wa Baraza ya kata ya Kisukuru.

“Nina agiza makatibu wa matawi wote na wajumbe wa mabaraza kuwatumia wajumbe wa mashina katika kuongeza wanachama wenu Chama cha Mapinduzi jeshi lake la ushindi ni UWT hivyo UWT tujipange kwa ajili ya ushindi kusonga mbele na mafiga matatu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan, Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Ladslaus Kamoli na Diwani wetu Lucy Lugome wa Kisukuru ” alisema Diwani Semeni

Wakati huo huo aliwataka Wanawake wa UWT kuchukua fomu katika uchaguzi wa Serikali za mitaa wasijirudishe nyuma kwani uongozi unapangwa na Mwenyezi Mungu wajipime kama wanatosha wachukue fomu katika uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2024.

Diwani Semeni aliwataka umoja wanawake UWT Kisukuru kuwaunga mkono wanawake wenzao walio madarakani, Rais Dkt.Samia, Mbunge Bonah na Diwani Lucy Lugome wanachapa kazi na kutekeleza Ilani ya chama cha Mapinduzi vizuri

Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Kisukuru Bakari Mjema amewataka Umoja wanawake UWT kujenga umoja na Mshikamano katika kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa waache kuweka makundi .

Mwenyekiti wa umoja wanawake UWT Kata ya Kisukuru Dkt.Mery Mdegipara aliwataka UWT kata Kisukuru na Wajumbe wa Baraza kushirikiana na Diwani Semeni mtoka katika kujenga jumiya hiyo iweze kusonga mbele.

Dkt Mery alisema yeye na Jeshi lake la UWT wamejipanga vizuri na Chama kuakikisha ccm inashika dola katika chaguzi zake zote ikiwemo Uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa Rais wabunge na madiwani mwaka 2025