Na Israel Mwaisaka, Timesmajira Online-Nkasi
DIWANI wa Kata ya kala wilayani Nkasi mkoani Rukwa, Privatus Yoramu,amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi .
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Nkasi,Richard Maasai,amesema tukio hilo limetokea Jumatano ya Januari 28,2026majira ya saa 12 jioni wakati Privatus akipatiwa matibabu katika hospitali ya Mkoa ya Rukwa.
Amesema kuwa marehemu amefariki kutokana na ugonjwa wa kiharusi uliosababishwa shinikizo la juu la damu (Pressure) lililokuwa limempata na kusababisha mishipa ya damu na kusababisha kufikwa na umauti.
Masaai amefafanua kuwa juzi,kabla ya kufikwa na umauti Privatus aliongoza kikao cha kamati ya elimu na afya kama Mwenyekiti na akiwa katika kikao hicho alizidiwa na ugonjwa na kukimbizwa katika hospitali ya Wilaya Nkasi ambapo alipewa huduma ya awali na kukimbizwa katika hospitali ya Mkoa kwa matibabu zaidi .
Hata hivyo amedai kuwa mazishi ya Diwani huyo yatafanyika Jumamosi ya Januari 31,2026 katika Kijiji cha Kilambo Mkolechi Kata ya Kala.

More Stories
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi
Kihongosi:Uhai wa chama mashina