January 15, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Diwani awasilisha ilani ya utekelezaji

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

DIWANI wa Kata ya Pugu Imelda Samjela, amewasilisha Taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM ya January mpaka Desemba 2023.

” Nimewasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani katika uongozi wangu nimesimamia mambo mbali mbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa kituo cha afya Pugu Kajiungeni ni miongoni mwa vituo vya afya vya Serikali katika halmashauri ya jiji la Dar es Salaam kipo katika kata ya Pugu mtaa wa Bombani kinahudumia wakazi 49,422 wanaotoka katika mtaa mitano kata ya pugu na kata jirani zote ni juhudi ya Serikali “alisema Imelda.

Diwani Imeda Samjela akizungumzia barabara Barabara ya Pugu Majohe imejengwa kwa kwa kiwango cha Lami,changarawe,na mitaro ya zege na karavati,Barabara ya Kinyamwezi kimani kwa Frida imejengwa kwa kuchongwa Kalavati kuweka vifusi sehemu korofi na ujenzi wa daraja na barabara ya Kibog’wa imechongwa,Barabara ya Pugu Mwakanga imechongwa wameweka Kalavati,na vifusi sehemu korofi.

Aidha alisema vipaumbele vya jumla kata ya Pugu Barabara mtaa wa Bombani barabara ya Samjela kiwango cha Changarawe, mtaa wa mstapha Kibog’wa kiwango cha Changarawe.

Akizungumzia mafanikio makubwa yalipata kata Pugu baadhi yake ambayo yamefanywa na Serikali wakazi zaidi ya 52,800 wanapata maji safi na salama kutokana na uwepo wa huduma ya maji ya DAWASA .

Diwani Imelda alisema ujenzi wa mradi mkubwa Bangulo unaendelea Mkandarasi yupo site mradi ukikamilika mgao wa maji utaisha,thamani ya mradi bilioni 40 ambapo kwa sasa elimu kwa wadau, wateja inaendelea kutolewa kuhusiana na kulinda miundombinu ya maji.

Aliomba DAWASA waongeze juhudi katika usambazaji wa mabomba ya maji,hasa maeneo ambayo bado hayajafikiwa na huduma kwenye mitaa ya Mstapha, Kinyamwezi, ili kumaliza kabisa kero ya maji

Akizungumzia changamoto mbalimbali za kata ya Pugu ikiwemo daraja la Kinyamwezi, limekata mawasiliano wananchi wanapita Buyuni,aliomba Serikali iwajengee Daraja mpya pia wanaitaji daraja la Mtaa Kinyamwezi ambapo ni mtaa mkubwa.