January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Diwani Cheka awataka waumini kushiriki katika Daftari la mpiga kura

Na Heri Shaaban, TimesMajira Onlien

DIWANI wa Viti Maalum Wanawake wilaya ya Ilala Magreth Cheka ,amewataka waumini wa Kanisa la MOROVIAN Ukonga Kushiriki kujiandikisha katika Daftari la mpiga kura ili waweze kupata haki yao ya Msingi waweze kumpigia kura kiongozi wa Serikali za mitaa wakati wa Daftari la mpiga kura likifika ili waweze kuchagua viongozi bora.

Diwani Magreth Cheka , alisema hayo katika ibada Maalum ya kuchangia Kwaya ya Kanisa la Morovian Ukonga Majumba sita katika ibada Maalum.

“Naupongeza uongozi wa Kanisa hili la Morovian kwa Mshikamano wenu pamoja na Kwaya ya Kanisa hili
Nawaomba mdumishe AMANI katika nchi yetu na kukuombea Dua Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anazofanya” alisema Cheka

Diwani Magreth Cheka alisema yeye ni Muumini wa Kanisa Katoliki lakini amevutiwa na waumini wa Kanisa la Morovian kwa kushiriki ibada pamoja katika kanisa hilo.