Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
DIWANI wa viti Maalum Wanawake wilaya ya Ilala Magreth Cheka ,ambaye ni Mlezi wa Kata ya Kivule, amewataka wanawake wa uwt kivule kuunda vikundi vya Wanawake kwa ajili ya kupata mikopo ya Serikali ambayo inatarajia kufunguliwa rasmi julai mwaka huu.
DIWANI Magreth Cheka,alisema hayo katika mkutano wa umoja wanawake UWT tawi la Mji mwema Kivule Wilayani Ilala, mkoa Dar es Salaam.
“Naomba wanawake wa UWT Kivule muunde vikundi vya wanawake kwa ajili ya mikopo ya Serikali mjikwamue kiuchumi hivi karibuni mikopo hiyo itatoka rasmi hivyo kila kikundi cha mkopo kifuate taratibu ikiwemo kujisajili katika mfumo wa mtandao ukiwa na vitamburisho vya NIDA “alisema Cheka.
Aliwataka Wanawake wa kivule kushirikiana na Mama Maendeleo wa kata kwa ajili ya kupewa elimu ya usajasiriamali na taratibu za usajili wa kisasa .
Aliwataka makatibu wa Vikundi vya vikopa kushirikiana na Afisa Maendeleo ya kata ya Kivule kwa ajili ya mchakato wa kusajili vikundi vyao ili viwe katika taratibu za kupata mikopo hiyo ya asilimia kumi ambayo inatoleqa ngazi ya Halmashauri zote nchini .
Alisema mikopo ya Serikali aina riba hivyo wachangamkie fursa ya kukopa ili wakuze mitaji yao sambamba na kufanya marejesho katika taasisi za Benki ambazo watapangiwa kuchukua mikopo hiyo na taratibu wataelezwa .
Aidha alitaka kila wanawake wa vikundi vya mkopo kufamiana ili kuondoa usumbufu wakati wa marejesho.
KATIBU wa umoja wanawake UWT Mji Mwema Kivule Sarah Isesha, alisema tawi la UWT Mji Mwema lina wanawake wa UWT 260 wanachama wa ccm 270 kati yao wenye kadi za mpiga kura 143 na wenye namba za NIDA 140 mikakati yao kuongeza wanachama kufikia 500 .
Katibu Sarah alisema mikakati yao mingine uwt Mji Mwema kwa kuongeza wanachama na kusajili katika mfumo wa kadi za kisasa la electronic .
Akizungumzia changamoto za Tawi la UWT Mji Mwema miundombinu ya Barabara pamoja na Mkopo ya Serikali vikundi vya wanawake wa eneo hilo mikopo aijawafikia.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba