November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ditopile amlipua Lema, amtaka ajitokeze kuomba radhi

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Dodoma Mhe Mariam Ditopile amemtaka aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Godbless Lema ajitokeze aombe radhi kutokana na kauli yake aliyoitoa kuhusu Vicoba ambayo ni yakuwadhihaki wanawake.

Katiba hotuba yake Lema alikaririwa akisema Vicoba ni umasiki na ndio maana alimwondoa mkewe kwenye benki hizo.

Ditopile ametoa wito huo alipo kuwa mgeni rasmi katika kongamoano la Vicoba na kumpongeza Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza miaka miwili madarakani liloandaliwa na Shirika la Msaada wa Kisheria (JUST).

“Kama kweli tunataka kurekebisha pale ambapo serikali imekosea basi tuwe na lugha nzuri,kama kuna mtu anaona vikoba havifai basi aje na hoja zake sio kudharau kwasababu wapo wanawake wengi wanaendesha shughuli zao kupitia fedha hizo kidogo”

Amesema “Ndugu yangu huyu Godbless Lema kiukweli ametumia lugha ambayo imetudhihaki sisi wanawake na inawezekana hata mama yake alikuwa ni miongoni na kama anahoja aishauri serikali”

“Mimi namuomba ashuke chini akafuatilie vikoba hivi ni kwa namna gani vimeinua maisha ya watanzania ajifunze na kama anaona kuna sehemu ya kujirekebisha aseme, ikiwezekana atoke na afute kauli yake kwasababu ametukosea sana, asitumie uhuru vibaya aliopewa na Rais Dkt. Samia”

Ditopile amesisitiza kuwa uanzishwaji wa huduma ndogo za fedha upo kwa mujibu wa sheria ambayo ilitungwa wakati Godbless Lema akiwa Mbunge.

Alisema wizara ya fedha ilitunga sheria ya huduma ndogo za fedha mwaka 2017 lengo ni kuhakikisha huduma hiyo inaleta tija kwa wananchi.