December 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Diddy, Cassie wamalizana kwa amani nje ya mahakama

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

WASANII wa muziki wa rap Sean “Diddy” Combs na wa R&B Casandra “Cassie” Ventura wamemalizana nje ya mahakama siku moja baada Cassie kumshtaki Diddy kwa ubakaji na unyanyasaji wa kingono.

Kwa mujibu wa mtandao wa BBC News, wawili hao wamefikia makubaliano ijumaa japo hawakutoa maelezo yoyote kuhusu makubaliano hayo.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotelewa na wawili hao kwa pamoja imesema kuwa Ventura amekubali kumaliza shauri hilo kwa amani na kwa masharti yanayompa udhibiti.

“Napenda kuwashukuru familia yangu, mashabiki na wanasheria wangu kwa msaada wao usioyumba.” Alisema Cassie

Kwa upande wake Sean “Diddy” Combs alisema “tumekubaliana kuyamaliza kwa amani. Namtakia Cassie na familia yake kila mafanikio, upendo”

Ni jana tu mtandao wa TimesMajira ulirripoti taarifa ya kesi iliyofunguliwa na Casandra “Cassie” Ventura akimshtaki  Sean “Diddy” Combs akidai alinyanyaswa kwa miaka 10 katika uhusiano na aliyekuwa mpenzi wake, Diddy.

Hata hivyo msanii huyo wa Rap ambaye pia ni maarufu kwa jina la Puff Daddy, alikanusha madai hayo na kudai kuwa mwimbajii huyo wa miondoko ya RnB anajaribu kumuibia. Mwanasheria wa Diddy anasema kuwa mashtaka hayo yanaudhi na kuchukiza.

Akidhibitisha makubaliano hayo, mwanasheria wa Cassie, Douglas Wigdor alisema “nimefurahishwa sana na Ventura kwa kuwa na nguvu ya kupambana na shauri hili. Anastahili poongezi kwa kufanya hivyo”