Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
MWANAMUZIKI na producer maarufu katika ulimwengu wa RnB na Hiphop, Sean Combs “Diddy” ameshitakiwa katika mahakamani, akimtuhumiwa na mpenzi wake wa zamani kwa ubakaji na unyanyasaji wa kimwili kwa muda mrefu.
Kwa mujibu wa mtandao wa Gazeti la Independent, mwanamuziki wa miondoko ya RnB, Casandra Ventura “Cassie” amefungua kesi dhidi ya mpenzi wake wa zamani Diddy, akimshutumu mkali huyo wa hip-hop kwa ubakaji na unyanyasaji wa kimwili mara kwa mara katika uhusiano wao wote.
Kulingana na hati za mashtaka, mwimbaji wa wimbo maarufu “Me & U” – Cassie alidai kwamba alikutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Revolt (Diddy) mwaka 2005 akiwa na umri wa miaka 19 na kudai alianza kumnyanyasa kimwili ambapo ni pamoja na madai ya kumlazimisha kufanya ngono na makahaba wa kiume huku akipiga picha na kumpa dawa za kulevya.
Cassie pia alidai katika shauri hilo kwamba Sean Combs , alidaiwa kwa mara kadhaa kumuingilia nyumbani kwake na kumbaka katika nyakati za mwisho wa uhusiano wao kipindi cha mwaka 2018.
Kama haitoshi kwa mujibu wa mtandao wa TMZ Tv, imeripotiwa kuwa Polisi wa New York (NYPD) kufanya uchunguzi mkali dhidi ya Diddy kwa madai kuwa anahusishwa na unyanyasaji wa kingono.
Vyanzo vya ndani kutoka polisi vimeeleza kuwa kumefunguliwa madai ya wazi kumhusisha Sean Combs, hata hivyo nyaraka hizo zimefungiwa, na kutowekwa wazi mlalamikaji mashtaka hayo ni nani.
More Stories
Startimes yazindua makala ya China, Africa
Jay-Z aunganishwa na P Diddy kwa kumdhalilisha binti wa miaka 13
Mwanasheria wa Katavi aliyetimkia kwenye muziki achaguliwa tuzo za MIEMMA