December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Diamond, Zuchu, Nandy wafanya kweli tuzo za Afrimma

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

WASANII wa tatu hapa nchini katika muziki wa Bongo fleva, Bosi wa Wsafi Media Naseeb Abdul ‘DiamondPlatnumz’, Zuhura Kopa ‘Zuchu’ na Faustina Charles ‘Nandy’ wamefanikiwa kushinda tuzo za Afrimma zilizofanyika usiku wa kuamkia leo

Tuzo hizo hutafuta wasanii waliofanya vizuri kwa mwaka kupitia kazi zao kama zilivyo tuzo zingine na baadhi ya wasanii walipata nafasi ya kutajwa/kuwania tuzo mwaka huu wengine kutoka Tanzania na mataifa mengine barani Afrika.

Tanzania wamepata nafasi wasanii watatu tu. Ambapo Diamondplatnumz ameshinda tuzo ya Msanii Bora wa kiume Afrika Mashariki ‘Best male East Africa’, Zuchu ameshinda tuzo ya Msanii bora chipukizi ( Best Newcomer) huku Nandy akishinda tuzo ya Msanii Bora wa kike Afrika Mashariki ‘Best Female East Africa’.

Mbali na wasanii hao, wengine walioshinda nje ya Tanzania ni Masterkgsa amabye wimbo wake aliomshirikisha Nomcebo_zikode ‘Jerusalema’ umechaguliwa kuwa wimbo Bora wa Mwaka (Song of the Year) huku Rema akishinda tuzo ya ‘Best Male West Africa’.

Nyota wa muziki kutoka chini Nigeria Symplysimi, ameshinda tuzo ya ‘Best Female West Africa’ lakini pia Msanii wa muziki kutoka Nchini Congo Fallyipupa01, ameshinda tuzo ya ‘Best male Central Africa’, huku Nasty C kutoka Afrika Kusini akishinda tuzo ya Rapper bora wa mwaka.