December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Diamond: Sikuwafundisha Harmonize na Rayavanny kupelekana polisi

Na Mwandishi Wetu,TimesMajira Online

MSANII wa muziki wa Bongo fleva na Bosi wa Wasafi Media, Diamond Platnumz amechukizwa na mambo yanayoendelea kati ya msanii wake Rayvanny na aliyewahi kuwa msanii wa lebo yake, Harmonize kupelekana Polisi.

Harmonize na Rayvanny kesi yao ipo Polisi kutokana na Harmonize kushtaki kuwa anachafuliwa kwa baadhi ya picha zake za utupu kusambaa mitandaoni.

Katika sakata hilo, Harmonize aliwashitaki wote waliohusika kusambaza picha hizo huku akiwashuku Rayvanny, Baba levo, Paula mtoto wa Kajala na Kajala mwenyewe.

Akizungumzia hilo, Diamond amesema, anachotaka kuona ni kusikia wanamuziki hao wananshindana kwenye kazi na sio mambo yasiyohusu kazi, huku akisema yeye hakuwafundisha kupelekana Polisi,

“Sijafurahishwa kusikia wanapelekana Polisi, Waige mifano ya sisi kaka zao, mfano mimi na Alikiba hatukuwahi kuepelekana polisi tulikuwa tunashindana kupitia kazi zetu tu,” alisema Diamond.