Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
MSANII wa muziki wa Bongo fleva na Bosi wa Wasafi Media hapa nchini Diamondplatnumz, amefarijika na zawadi atakayepewa mshindi wa sanaa ya cheka.tu Comedy Search ambaye licha ya kupewa milioni 10, ajira, na zawadi mbalimbali, lakini pia atapewa na Kiwanja.
Akizungumzia hilo kupitia kwenye Ukurasa wake wa Instagram Diamond amesema, kwa kufanya hivyo ni jambo jema jema kwa vijana wenzetu kwasababu mshindi anakuwa na uhakika wa ajira, makazi lakini pia na pesa ya kujikimu kimaisha.
“Kwanza kabisa, nimpongeze Coy Mzungu na Wana Cheka.tu wote kwa kuendelea kuikuza na kuiheshimisha tasnia ya Standup Comedy. Lakini niwashukuru tena wao na team nzima ya Wasafi Tv na Wasafi Fm kwa kutengengeneza Platform hii ambayo naamini itaenda kuzalisha vipaji, ajira na kubadili maisha ya vijana mbalimbali toka mtaani.
“Binafsi, hii Cheka tu Comedt Search ni moja ya vitu ambavyo nilikuwa navisubiri kwa hamu, kwasababu nafahamu jinsi watanzania wamejaliwa vipaji mbalimbali. Tafadhali naomba nitagie wote wenye vipaji vya uchekeshaji hapa na pia hakikisha Unafuatilia wasafitv na wasafifm ili kujua kila hatua, maana naamini huu ni wakati wako. List ya Majaji inatosha kusema kuwa mshindi atakua mwenye kipaji na wa halali haswa!,” amesema Diamond.
%%%%%%%%%%%%%%
More Stories
Startimes yazindua makala ya China, Africa
Mwanasheria wa Katavi aliyetimkia kwenye muziki achaguliwa tuzo za MIEMMA
Coca-cola ‘Kitaa Food Fest’ yahitimishwa kwa mafanikio