Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
MSANII wa muziki wa Bongo fleva na Bosi wa Wasafi Media Naseeb Abdul maarufu ‘Diamond Platnumz’, leo ameachia wimbo mpya ujulikanao ‘Waah!’ aliomshirikisha mkongwe wa muziki wa dansi kutoka nchini Congo Koffi Olomide.
Wimbo huo umeachiwa katika ofisi za Makao Makuu ya Wasafi Media ambapo Koffi Olomide amepata nafasi ya kuangalia namna ya utendaji na uzalishaji wa vipindi unavyofanyika katika Media hiyo akiongozana na mwenyeji wake Diamond Platnumz.
Hata hivyo, Koffi amesifia namna ambavyo kuna mipango kazi mizuri ndani ya Wasafi Media, lakini pia akimpongeza Diamondplatnumz kwa kuweza kutoa nafasi ya ajira kwa vijana zaidi.
More Stories
Startimes yazindua makala ya China, Africa
Mwanasheria wa Katavi aliyetimkia kwenye muziki achaguliwa tuzo za MIEMMA
Coca-cola ‘Kitaa Food Fest’ yahitimishwa kwa mafanikio