December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Diamond Platnumz

Diamond azindua Kampeni ya Wasafi Tumekiwasha na Tigo

a Mwandishi Wetu, TimesMajir Online

MSANII wa muziki wa Bongo fleva na Bosi wa Wasafi Media Naseeb Abdul maarufu ‘Daimond Platnumz’, leo amezindua ‘Kampeni ya Wasafi Tumekiwasha na Tigo’, ambayo inatarajia kufanyika Novemba 28 mwaka huu mkoani Shinyanga.

Kampeni hiyo ambayo imeandaliwa na Kampuni ya Wasafi Media kupitia vituo vyake inatarajia kufanyika katika mikoa saba ambayo masafa ya kituo hicho yamezinduliwa.

Kupitia kampeni hiyo waandaaji na watagazaji wa vipindi kutoka Wasafi Media watapata fursa ya kukutana na wananchi wa mikoa hiyo kama njia ya kushererekea mafanikio yao toka kuanzishwa kwa kituo hicho.

Akizungumza katika hafla iliyofanyika Makao makuu ya Ofisi hizo Jijini Dar es Salaam Daimond amsema, kampeni hiyo itawahusisha watagazaji, waandaaji wa vipindi pamoja na wasanii mbalimbali kama njia ya kushererekea mafanikio mbalimbali pamoja na wananchi tangu kuanzishwa kwake.

Diamond ametaja mikoa ambayo Kampeni hiyo itafanyika kuwa ni Shinyanga, Mbeya, Arusha, Dodoma, Mwanza, Zanzibar, pamoja na Dar es salaam.

” Kampeni hii inatarajia kufanyika katika mikoa saba ambayo itajumuisha wakazi wa maeneo hayo kama njia ya kujadili kwa pamoja mafanikio na fursa zinazopatikana katika mikoa hiyo, “amesema Daimond Platnumz

Kwa upande wake William Mpinga, Mkuu wa kitengo cha Masoko amesema, ‘Kampeni ya Wasafi Tumekiwasha na Tigo’ ni jukwaa sahihi la kuwauganisha watanzania kwa pamoja kushererekea mafanikio ya Wasafi Media na Tigo kupitia kampeni yake ya jaza tukujaze tena.