Na Judith Ferdinand,Timesmajira Online,Mwanza
Jeshi la Poli Mkoa wa Mwanza limefanikiwa kumkamata Oswald Kaijage Binamungu mwenye umri wa miaka 39 Mhandisi wa umeme katika mgodi wa Geita Gold Mining(GGM), aliyetoroka baada ya kusababisha ajali siku ya Jumamosi Julai 22,2023 eneo la Lumala barabara ya Kiseke wilayani Ilemela mkoani Mwanza.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza SACP. Wilbrod Mutafungwa amesema kuwa ajali hiyo ilihusisha gari yenye namba za usajili T.476 DZL aina yaToyota Hilux Double Cabin kwa kuwagonga watu waliokuwa wanafanya mazoezi ya mchakamchaka kikundi cha kukimbia cha Aden Palace(jogging club) katika barabara hiyo.
Ambapo alisababisha vifo vya watu sita na majeruhi wanaondelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sekou Toure na ya Rufaa ya Kanda Bugando ambapo katika hospitali ya Sekou Toure wamebaki majeruhi 4 na Bugando 5 hali zao za kiafya zinaendelea kuimarika.
Mutafungwa amesema kuwa jeshi hilo mkoani Mwanza linaendelea kuvikumbusha vikundi vya mchamchaka kusajili vikundi vyao kwenye ofisi za utamaduni katika ngazi ya Wilaya ,Manispaa ay Jiji ili wapewe miongozo au maelekezo ya namna bora ya kufanya mazoezi na kuzingatia hali ya usalama wao na watu wengine.
“Vikundi hivyo endapo vinahitaji kutumia barabara wakati wa mazoezi yao tunavikumbusha kutoa taarifa kwa jeshi letu katika wilaya husika ili askari wa usalama barabarani waweze kusimamia usalama wao na watumiaji wengine wa barabara ambao kwa wakati huo watakuwa wanatumia barabara hizo ili kuepusha ajali,”.
Sanjari na hayo jeshi hilo mkoani Mwanza limewaita viongozi wote wa jogging club siku ya Jumamosi Julai 29 mwaka huu majira ya saa moja asubuhi katika uwanja wa michezo Nyamagana ili kufika kwa ajili ya kupata elimu zaidi ya usalama barabarani na mambo muhimu wanayotakiwa kuzingatia wawapo barabarani wakati wakikimbia ili kuepusha ajali.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba