Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online
Kamishna Jenerali wa kuzuia na kupambana na dawa za nchini, Gerald Kusaya amewaonya wasanii wanaotumia na wanaohamasisha matumizi ya dawa za kulevya kupitia nyimbo zao akiahidi hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
Aidha,washirika wa mmiliki wa kituo cha Cambiasso Sport Academy kilichopo Tuangoma wamekamatwa na kilo 15 za dawa za kulevya aina ya heroine, Watuhumiwa hao waliokamatwa ni Suleiman Thabit wa Salasala, Sharifa Suleiman Bakari wa Maji Matitu na Farid Hamis Said mkazi wa Maji Matitu Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Kusaya ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari akibainisha kuwa Mamlaka hiyo imefanikiwa kuwakamata watu wanne wakisafirisha dawa za kulevya kwenda nje ya nchi.
More Stories
Wanafunzi 170 wapata ufadhili wa masomo
Maelfu kunufaika namsaada wa kisheria Katavi
Serikali yazidi kuwakosha wawekezaji wadau waipa tano