July 3, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

DCEA yawanoa waandishi wa habari kuhusu kemikali bashirifu

Na Mwandishi Wetu,Timesmajira Online

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), imewanoa waandishi wa habari nchini kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu mapambano dhidi ya biashara haramu ya dawa za kulevya ikiwemo kemikali bashirifu.

Mafunzo hayo yamefanyika leo Julai 3,2026 jijini Dar es Salaam, lengo likiwa kuwajengea uwezo wa kuihabarisha jamii kuhusu dawa tiba zenye asili ya kulevya, dawa mpya za kulevya& Maabara Bubu pamoja na Madhara ya Dawa za kulevya.

Akitoa mada kuhusu kemikali bashirifu na dawa za kulevya, Kamishina Msaidizi wa Uchunguzi kutoka DCEA, Ziliwa Machibya amezitaja Sheria ya kemikali za Viwandani na Majumbani (Udhibiti na Usimamizi) Na. 3 ya Mwaka 2003.

Nyingine ni Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Na. 5 ya Mwaka 2015 (R.E 2020), Vifungu vya (14, 15, 15A) pamoja na Sheria ya Dawa na Vifaa Tiba Na. 1 ya Mwaka 2003 marekebisho ya Sheria ya Fedha 2019).

Amesema, kutokana na sheria hizo ametaja kemikamili bashirifu zilizokamatwa maeneo mbalimbali duniani ni Acetone lita 3360, Ethanol – lita 8750, Azobisisobutyronitrile – kilo 60, Hydrochloric Acid kilo 1400, Lead acetate kilo 5000, N-methylformamide-lita 1890.

Dawa nyingine ni Toluene lita 420, Tartaric acid kilo 375, (2-bromoethyl) benzene kilo 13.5, acetic acidi kilo 4.4, Acetone kilo 22.5, benzyl alcohol kilo 434, ethanol kilo 358, hydrochloric acid 1834.36, methylamine 202.5, tartaric acid kilo 21, toluene kilo 67.5.

Akitoa mifano ya Uchepushwaji nchini, Machibya amesema uchunguzi ulibaini kiasi cha kilo 12 za kemikali bashirifu aina yapseudoephedrine zilikuwa zimechepushwa katika mchakato wa uzalishaji wa dawa za kikohozi na kupelekea uteketezaji wa lita10,000 za dawa zenye pungufu ya kiambata hai cha kemikali hiyo

Pia, amesema ukamatwaji wa tani 21.7 za acetic anhydride nchini Pakistani zilizosafirishwa kutoka Tanzania kwa jina bandia la acetic acid

“Mwaka 2025, jumla ya tani 31.76 na lita 183.500 zà kemikali bashirifu zilikamatwa hapa Nchini. Zimezuiliwa kemikali bashirifu tani 734 Kuingia nchini kinyume cha taratibu.

“Kiasi hiki kinahusisha tani 4 za kemikali bashirifu za kutengeneza dawa ya kulevya aina ya fentanaili (kilipangwa kusafirishwa Kwenda Mexico kwa jina bandia la protein biotine).

“Pia, kugundulika kwa maabara bubu ya kutengeneza methafetamine mpakani Namanga upande wa Kenya,” amesema Machibya.