May 31, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

DC Ubungo kuanza kuwasajili ‘bodaboda’

Na Heri Shaaban,Timesmajiraonline,Ubungo

MKUU wa Wilaya ya Ubungo Albert Msando,amesema mikakati yake katika wilaya ya Ubungo ni kuitambua sekta isiyo rasmi ya Waendesha Pikipiki maarufu bodaboda kwa kuwasajili  kuwapatia vyeti vya kuzaliwa na vitamburisho vya Taifa NIDA ili waweze kupewa leseni za udereva waweze kumiliki Pikipiki zao.

Msando amesema hayo jijini hapa leo Mei 29,2025 wakati akizungumza kwenye mkutano wa vyama vya Ushirika Mkoa Dar Es Salaam.

“Mikakati yangu mwezi huu tunatarajia kuwasajili waendesha bodaboda wa Ubungo wote waweze kupata vyeti vya kuzaliwa watengeze NIDA yao waweze kupata leseni wamiliki Pikipiki zao watoke katika biashara ya kuajiliwa kwa mkataba inawanyonya,”amesema Msando.

Amesema anatoa maelekezo hayo kwa watendaji wake wa wilaya ya ubungo waanze kutekeleza mara moja ili vijana wa bodoboda wapate fursa  hii haraka wakuze uchumi ushirika wao ukue.

Alisema waendesha bodaboda wa Ubungo kupitia ushirika huo wakiwa na NIDA, TRA na vyeti vyao vya kuzaliwa ni Rais kutambulika waweze kukopa mikopo ya ushirika au mikopo ya Serikali kwa kuwa wanatamburika rasmi 

Amesema sekta hiyo isiyo rasmi ya bodaboda wanafanya kazi ngumu wengi wao hawana leseni hivyo wanafanya kazi kutegemea mikataba ya unyanyaaaji kutoka kwa mabosi wao.

Aliwataka maafisa maendeleo wa kata Ubungo na Maafisa watendaji kata jukumu lao kwa sasa kuwatambua vijana hao ambao ni watu muhimu na wana mchango mkubwa kwa jamii na Serikali.

Alitoa agizo kwa vyama vya ushirika kuwatumia bodaboda ni watu muhimu katika sekta ya kukuza uchumi wa nchi yetu hivyo wana ushirika kuwatumia vizuri kuwapa elimu waweze kutekeleza majukumu yao kwani vijana wengi wa bodaboda asilimia 93 wanalipwa shilingi 300,000 ila hawana mikopo ya Serikali .

Akizungumzia sekta ushirika alisema alitoa wito kusimamia vyema sekta ya ushirika na kuzitaka kampuni za simu zisiwabane wana ushirika kutokana na mikopo hiyo kutokana na riba zao katika utekelezaji wa majukumu yao 
Alivitaka vyama vya ushirika mkoa wa Dar es salaam kusimamia vyema sekta ya ushirika na kuzitaka kampuni za simu zitekeleze majukumu yao ya simu waache mambo ya songesha na kuwadai pesa wananchi.

Aidha aliagiza matumizi ya Mfumo wa Digitali TEHAMA utumike kwa vyama ushirika vyote kwani Dunia kwa sasa ipo katika mfumo huo  .

Alizitaka kampuni za simu zisiwabane wana ushirika kupitia mikopo ya simu za mkononi kutokana na kuwepo kwa riba kubwa .

Katika hatua nyingine amevitaka vyama vya ushirika visibague vyama vya chini kutokana na mitaji yao kuwa midogo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jukwaa la Ushirika Mkoa wa Dar es Salaam,Enerest Nyambo, amesema kuwa jukwaa hilo ni la nane kufanyika na lina lengo la kutoa suluhisho kwa changamoto zinazowakabili waajiri na waajiriwa katika maeneo yao ya kazi.

“Tuna ufadhili kutoka taasisi mbalimbali za kifedha kupitia jukwaa hili, tunapokea maelekezo ya viongozi wa serikali na kuyatekeleza kwa wakati.

Nyambo alisema wanahimiza wanachama wa vyama vya ushirika kufuata taratibu zote zinazohusu utoaji wa mikopo

Pia alisema  Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika mkoa wa Dar es Salaam, limelenga kuweka mikakati ya pamoja ili kuboresha huduma kwa wanachama na kuchochea maendeleo ya kiuchumi kupitia ushirika.