Na Mwandishi Wetu,TimesMajira
MKUU wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka, amefanya ziara ya gahafla katika Stendi Kuu ya Mabasi ya Kilosa kwa lengo la kusikiliza kero, changamoto na maoni ya wafanyabiashara, waendesha bodaboda, wajasiriamali na wananchi wanaopata huduma katika stendi hiyo.
Katika ziara hiyo, Shaka alitembea huku na huko ndani ya stendi, akizungumza ana kwa ana na wananchi bila itifaki, akisikiliza kero zao kuhusu usafi, ulinzi na usalama, utaratibu wa kupanga magari, maeneo ya biashara, pamoja na changamoto za miundombinu.
Wafanyabiashara na bodaboda waliishukuru serikali kwa hatua hiyo, wakisema ni mara ya kwanza kuona kiongozi anashuka chini moja kwa moja kuwasikiliza bila kupewa taarifa ya awali.

Akizungumza baada ya kusikiliza kero hizo, Mkuu wa Wilaya amesema:
“Nimekuja hapa sio kama mkuu, nimekuja kama mtumishi wenu. Uongozi ni kusikiliza, sio kukaa ofisini. Kila kero mloyonieleza leo nimeipokea, na nitahakikisha tunaitatua kwa kushirikiana na Halmashauri na wadau wote. Stendi hii ni sura ya Kilosa, lazima iwe safi, salama na yenye heshima kwa mteja.” Shaka
Aidha, Shaka ameagiza Halmashauri na uongozi wa stendi kushughulikia kwa haraka kero za dharura zilizojitokeza, huku akisisitiza kuwa mlango wake uko wazi kwa kila mwananchi.
Ziara hiyo imeacha faraja kubwa kwa wananchi wa Kilosa, ambao wamesema wameona uongozi wa vitendo unaogusa maisha ya watu wa kawaida.

More Stories
Wizara yatakiwa kutumia fursa za nje kukuza uchumi wa Taifa
Magesa awataka watendaji kufuata sheria ukusanyaji wa mapato
Chalamila kwenda Qatar kuishangilia Serengeti Boys