February 21, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

DC pogolo: Mapato ya Halmashauri kujenga Mahabara Kisukuru

NA HERI SHAABAN( ILALA)

MKUU wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, amesema Mapato ya Halmashauri ya Jiji yatakayoongezeka yataelekezwa Kata ya Kisukuru kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Mahabara ya kisasa na madarasa ya shule .

Hayo yalisemwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Kisukuru ulioandaliwa na Diwani Lucy Lugome, alipokuwa alielezea mikakati ya maendeleo.

“Makusanyo ya Halmashauri yakidhidi shilingi bilioni 120 tutapeleka kata ya Kisukuru kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Mahabara ya kisasa katika shule ya sekondari Serikali yetu ni sikivu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Dkt.Samia Suluhu Hassan “alisema Mpogolo.

Mkuu wa wilaya Edward Mpogolo ,aliwataka wananchi wa Kisukuru kuvuta subira Kisukuru itakuwa ya kisasa mara baada kukamilika barabara za kisasa zinazojengwa na Serikali.

Aidha alisema pia fedha nyingine watajenga watajenga shule ,ile. Shule ya zamani chakavu itavunjwa ili ikengwe ya kisasa.

Pia alisema shilingi milioni 500. Halmashauri imetenga kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya polisi kikiwemo cha Kisukuru ambapo kila kata kutakuwa na kituo cha Polisi.

Akizungumzia Mikopo ya Halmashauri itatolewa ya asilimia kumi aliwataka Wanawake ,vikundi vya Bodaboda,na watu wenye ulemavu wakakope ili uchumi wa nchi yetu uweze kukua .

Aliwataka wanawake wa Kisukuru kushirikiana na Diwani wa Kisukuru na Afisa Maendeleo ili waweze kupata mikopo ya Serikali pamoja na kutengeza KATIBA ya vikundi vinavyotambulika .

Katika hatua nyingine Mkuu wa wilaya Edward Mpogolo aliwaonya Wanawake wa Vikundi wasiende Steshenali kutengeza katiba ya mikopo gharama zake ni kubwa wawatumie maafisa maendeleo wa Serikali kwa ajili ya kutengeza vikundi na katiba.
Mwisho