October 7, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

DC : Ngorongoro kulipa fidia wananchi Ndolezi mwezi Machi

Na Mary Margwe, TimesMajira Online, Mbozi

Wananchi wa Kijiji cha Ndolezi Kata ya Mlangali Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe wanaodai kulipwa fidia kwa ajili ya kupisha maeneo ya karibu kilipo KIMONDO wanatarajia kulipwa fidia hiyo mnamo mwezi Machi, Mwaka huu 2023.

Hayo yalibainishwa juzi na Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Ester Mahawe, wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha kwenye Mkutano Mkuu wa hadhara.

Mahawe alisema fidia hiyo inaandaliwa tayari kuanza kulipwa na Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro, kazi itakayoanza mwezi Machi, na hivyo kuwataka wananchi kuvuta subira.

” February 12, Mwaka huu nilipata fulsa ya kutembelea Kijiji Cha Ndolezi Wilaya ya Mbozi, lengo likiwa ni kufanya Mkutano wa hadhara na wananchi wanaodai fidia kwa ajili ya kupisha maeneo ya karibu kilipo KIMONDO” alisema Mahawe.

“Fidia hiyo inaandaliwa tayari kuanza kulipwa na Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kuanza mwezi Machi, baada ya hapo tulipata nafasi ya kutembelea kilipo KIMONDO hiko, ambapo kwangu mimi ilikua ni fulsa ya kufanya utalii wa ndani” alisema Mahawe Mkuu wa Wilaya ya Mbozi.

Aidha alisema Kimondo hiko kipo katika Kijiji Cha Ndolezi Kata ya Mlangali, ambapo kiligundulika kutoka angani karibu na Mji wa Vwawa ambacho kinakadiliwa kuwa na uzito zaidi ya tani 12.

” Kimondo kilianguka katika kilima cha Mlenje, kipo kati ya vimondo vizito 10 vinavyojulikana duniani, kina urefi wa mita 3.3, upana wa mita 1.63 na kimo Cha mita 1.22, kina maumbile Maalum tofauti na vimondo vingine vinavyopatikana ulimwenguni Kwa kuwa hiki ni hasa cha chuma, chuma ni asilimia 90.45, nikeli asilimia 8.69, sulfuri asilimia 0.01 na fosfori asilimia 0.11 ya masi yake ” alisema Mahawe.

Hata hivyo alisema Wilaya ya Mbozi ina majimbo mawili Jimbo la Vwawa lenye Kata 18, na Jimbo mama la Mbozi lenye Kata 11 na kupelekea jumla ya Kata 29, yaliyogawanywa wakati wa uchaguzi Mkuu wa 2015.