December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

DC :Namna gani wakulima wanufaike kupitia tigo

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Mbeya

MKUU wa wilaya ya Ludewa Victoria Mwanzigwa ameiomba Kampuni ya Mawasiliano ya simu za mkononi Tigo kuelimisha wakulima wanavyoweza kunuifa na huduma za Tigo hasa katika uzalishaji wa mazao.

Mwanzigwa ameyasema hayo mkoani Mbeya akiwa katika ziara yake kwenye banda la Tigo kwenye maonyesho ya Kitaifa ya wakulima Nane Nane katika Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya .

“Tupo katika maonyesho haya ya Kitaifa ya wakulima hapa katika Viwanja vya John Mwakangale ambapo name nimepata nafasi ya kutembelea mabanda ambapo pia nimetembelea katika banda hili la Tigo,

“Nashukuru miongoni mwa elimu niliyopata ni pamoja na ‘product’ bidhaa  mpya ya tigo kuhusiana na masuala ya kilimo.”amesema Mwanzigwa

Ameiomba Kampuni hiyo iendelee kutoa elimu namna ambavyo wakulima wanaweza kunufaika kupitia vyama vyao vya wakulima (AMCOS).

“Ombi langu ni kuomba tuzidi kufahamishwa namna ambavyo wakulima kupitia vyama vyao vya ushirika AMCOS wanaweza kunufaika na huduma zinazotolewa na tigo kwa maana ya mikopo hasa kwenye uwezeshwaji wa pembejeo ili wakulima   waongeze  tija kwenye kilimo.

Kiongozi huyo ametumia fursa hiyo kuwataka tigo na wananchi kwa ujumla waendelee kujifunza na kutoa huduma hasa za kilimo kwa wakulima kwa maslahi mapana ya wakulima wenyewe na Taifa kwa ujumla.

“Hatua hiyo pia itakwenda kukuza ajira ,kukuza  uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ajira.”

Aidha ameishukuru kampuni hiyo kwa kupeleka mawasiliano katika eneo la Lupingu wilayani humo ambalo halikuwa na mawasiliano kabisa huku akitumia nafasi hiyo kuwakaribisha Tigo kwenye wilaya ya Ludewa kuendelea kuboresha za mawasiliano.