January 12, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

DC Mpogolo awataka walimu wakuu kutoa taarifa za walimu wenye maadili mabovu

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

MKUU wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, amewataka wakuu wa shule kutoa taarifa za Walimu wenye Maadili mabovu shuleni ili waondolewe ajira wawekwe walimu wengine.

Mkuu wa Wilaya Ilala Edward Mpogolo ,amesema hayo wakati wa kikao kazi na Wakuu wa Shule za Sekondari ,Waratibu Elimu kata na walimu wapya 150 wa ajira ya mkataba.

“Nina agiza katika wilaya yangu ya Ilala mambo matano muyazingatie muwe na maadili mema,mvae nguo kwa heshima ili wanafunzi wafuate tabia njema , msimamie majukumu yenu vizuri “alisema Mpogolo

Mkuu wa Wilaya Edward Mpogolo, aliwataka Walimu Ilala wasitumie kilevi chochote wawapo kazini kutekeleza majukumu yao ya kiutumishi ambapo aliagiza Wakuu wa shule kufatilia mwenendo wa Tabia mbaya za walimu wenye maadili mabovu na kuwatolea taarifa.

Aliwataka Walimu wa wilaya ya Ilala kuwa mfano wa kuigwa na kukuza taaluma shuleni ili sekta ya Elimu Ilala iweze kungara.

Aidha aliwataka walimu kwenda kujifunza na kuwajua watoto kwa kuzidisha upendo na kuacha kuwachapa bakora wanafunzi badala yake watumie kipaji chao kwa kujitoa kwao na kujua desturi za maeneo yao wanayofanya kazi , kutokana na watu wanaoishi eneo hilo kuijua jumuiya..

Wakati huo huo aliwataka walimu kuwajibika na kuwa WAZALENDO kwa TAIFA lao .na nchi yao ili waweze kuaminiwa na Serikali katika kusimamia kazi mbali mbali za kiserikali .

Katika hatua nyingine aliwataka Walimu kutii na kufuata sheria na taratibu kwa wakuu wao wa Shule wanazofundisha ili waweze kuaminika katika utendaji wa kazi zao na kuongeza ufaulu .

” Nawaonya muwaache michango ya Tuition, na mitihani ya majaribio shule kila siku bila kufuata taratibu suala la michango mpaka kibari kutoka ofisi yangu”alisema