Na Mwandishi wetu,Timesmajira
MKUU wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, ametoa maelekezo ya Serikali ya miaka mitano mpango mkakati wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya Edward Mpogolo ,amesema hayo katika mkutano wa wadau wa sekta zote wa Wilaya ya Ilala pamoja na madiwani ambapo walikuwa wakijadili mpango mkakati kuanzia mwaka 2026 mpaka mwaka 2030 .
” Katika mpango huu mkakati wa Serikali miaka mitano ijayo , Wilaya ya Ilala inategemea ugeni mkubwa hivyo mpango mkakati huu nawaomba mkatumie teknolojia vizuri katika sekta ya Elimu,sekta ya afya ,makusanyo ya mapato,Masoko na mawasiliano “amesema Mpogolo.
Mkuu wa Wilaya Edward Mpogolo aliwataka wakatumie teknolojia hiyo vizuri itasaidia kuwafahamu Watendaji katika muda wao wa kazi katika kutumia mawasiliano.
Pia amewataka Watendaji wa Halmashauri hiyo wakazingatie ukuaji wa jiji la Dar es Salaam na idadi ya watu wende kwa mazingatio sambamba na kuboresha miundombinu ya Barabara pamoja na kata za pembezoni kama Msongola ,Chanika,Buyuni Zingiziwa wakazingatie mawasiliano ya Barabara
Amesema Ilala wamepiga penati yao wamekuwa chagizo inaenda kuonyesha dira ambapo watasimama kifua mbele miaka mitano ijayo ambapo alitumia fursa hiyo kuwapongeza wandaaji wa mpango huo .

Meya wa Ilala Nurudini sheta amesema Ilala lazima wajipange katika mpango huo mkakati wa miaka mitano wataenda kusimamia yote.
Kwa upande Naibu Meya wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam John Ryoba Mrema ametaka Halmashauri ya jiji hilo kutenga maeneo ya vivutio vya utalii na kuyatangaza kwa ajili ya wageni Mbalimbali ili kuongezea mapato Halmashauri.

Naibu Meya John Ryoba Mrema, amesema jiji hilo lina maeneo mengi ya Utalii wa ndani ambayo yangeweza kutangazwa na kutambulika lakini wananchi hawayafaham.
Pia ameshauri yawekwe maeneo yakupimzika kwa ajili ya shughuli mbalimbali za wananchi na mikusanyiko wawe wanatumia kwa ajili ya kula chakula,shughuli mbalimbali na nyakati za sikukuu wananchi kufurahi ambapo alitolea mfano kama ilivyo Zanzibar.

More Stories
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi
Kihongosi:Uhai wa chama mashina
Kihongosi: Msigombane kwa itikadi za vyama