Na Heri Shaaban, TimesMajira Online,Ilala
MKUU wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, ameagiza Baraza la kuhifadhi Mazingira (NEMC )kuwakamata wasambazaji wa mifuko ya plastiki ndani ya Wilaya ya Ilala .
Mkuu wa Wilaya Edward Mpogolo, aliyasema hayo katika Kampeni ya Usafi ya pendezesha Dar es Salaam ambapo leo usafi ulifanyika Barabara ya Lumumba na Kariakoo.
“Naagiza NEMC na Taasisi mbalimbali kukamata wasambasaji mifuko ya Plastiki mshirikiane na Halmashauri katika kuwakamata wanaosambaza mifuko ya plastiki katika Wilaya yetu ya Ilala “alisema Mpogolo.
Mpogolo alisema NEMC inaendelea kukamata watu wote ambao wanaosambaza mifuko hiyo .
Akizungumzia kampeni ya usafi ya pendezasha Dar es Salaam wataendelea kupanda miti na masoko makubwa yote yatafungwa taa ili kuwapa fursa Wafanyabiashara waweze kufanya biashara zao vizuri .
Aidha akizungumzia usafi alisema changamoto iliyopo Kariakoo Wafanyabiashara hawajui umuhimu wa usafi wakati wa asubuhi baada kushiriki usafi wanafungua maduka yao ya BiasharaAlitoa agizo kwa Maafisa Afya wa Wilaya ya Ilala kuwachukulia hatua wachafuzi wa Mazingira wote .
Aliwapongeza waandishi wa habari na Wadau wa Mazingira wakiwemo Wakandarasi wa Usafi kwa kuendelea kuipendezesha Dar es Salaam .
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Jomaary Mrisho ,Mkoa wa Dar es Salaam Kampeni ya usafi ni tofauti na mikoani aliwapongeza Wananchi wa Mkoa huo waelewa wa kampeni hiyo .
Mkurugenzi Mrisho alisema jitihada za Halmashauri ya Jiji zitaendelea kuwa wasafi katika kuipendezesha Dar es Salaam .
Alisema sheria za Usafi zitakuwa endelevu Halmashauri ya Wilaya ya ILALA wachafuzi wa Mazingira kupitia sheria ndogo za Halmashauri .
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa