Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
MKUU wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amemwelekeza Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Elhuruma Mabelya, kuwasaka na kuwanasa wale wote waliokopa jumla ya sh. bilioni 17 katika halmashauri hiyo na kushindwa kurejesha ili wachukuliwe hatua .
Mkuu wa wilaya Edward Mpogolo alisema hayo katika mkutano wa hadhara wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa kata za vingunguti,mnyamani na buguruni mkoni Dar es Salaam .
“Pesa hizi za Serikali zilikuwa zinatolewa ngazi ya Halmashauri mikopo ya asilimia kumi mapato ya ndani kwa ajili ya wanawake vijana na watu wenye ulemavu hivyo wale wote waliokopa na kushindwa kurejesha kwa wakati sasa tunaomba pesa zirejeshwe ili wengine waweze kukopa”alisema Mpogolo.
Mpogolo alisema kuna baadhi ya viongozi wamejinufaisha na fedha hizo kinyume cha taratibu wametakiwa kurejesha kabla kuumbuliwa .
Pia alionya vikali kama kuna viongozi walijinufaisha na fedha hizo kinyume cha utaratibu kuzirejesha kabla ya kuwaumbua.
Aidha aliwataka watakaopata mikopo hiyo kutokurubuniwa na wajanja wachache kuchomekwa majina kisha kupewa mgao mdogo baada mkopo kutoka .
Mkuu wa wilaya Edward Mpogolo ameanza ziara yake ya kutatua kero za wananchi ndani ya wilaya Ilala nzima katika mikutano ya ndani na mikutano ya nje kuongea na wananchi
Alisema halmashauri ya jiji imetenga zaidi ya shilingi bilioni 10 kwa ajili ya mikopo ya Serikali kupitia halmashauri ambayo inatarajia kutolewa Mwezi October mwaka huu.
” hizi fedha zipo tayari katika akaunti ya jiji nimeelekeza wajasiriamali mama na Baba kishe na vikundi vya Bodaboda vipewe kipaumbele waweze kukopa kupitia benki ” alisema .
Alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu fedha hizo kuanza kutolewa ambapo awamu hii vikundi vyote vitakopa kupitia utaratibu mzuri Benki hivyo
wananchi wafuate taratibu
More Stories
Bodaboda wamchangia Rais Samia Mil 1 ya fomu ya Urais
HAYA HAPA MATOKEO YOTE FORM II NA DARASA LA IV
Ufaulu waongezeka matokeo ya Darasa la Nne na Kidato cha Pili