Na Heri Shaaban, Timesmajira Online,Ilala
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amepiga marufuku shughuli zote za kilimo katika bonde la Magole Kibeberu Kata ya Mzinga.
Mpogolo amepiga marufuku hiyo wakati wa ziara yake wilayani Ilala ya kutatua kero mbalimbali za wananchi, baada ya kukatika kwa daraja na kukata mawasiliano ya pande mbili.
“Wakati Mkandarasi anaendelea kuhakikisha mawasiliano yamerejea katika hali ya kawaida, utekelezaji wa agizo unaanza mara moja “amesema Mpogolo.

Sanjari na hayo,akizungumza na viongozi wa Serikali ya Mtaa, wananchi na baadhi ya wakulima, Mpogolo amesisitiza sheria za matumizi ya ardhi kwa kuzingatia mita sitini toka barabara inapoanzia.
Ameeleza athari za kilimo katika bonde hilo ni pamoja na kutanuka kwa mto, hali inayofanya kuhama katika njia yake ya asili na kusababisha maji kupita nje ya makaravati.
Ametumia nafasi hiyo kumwagiza Mkandarasi kuhakikisha anazibua njia zote za maji ili kurudisha mifumo sahihi ya maji.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mzinga, Isac Job, amemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa hatua za haraka alizochukua kuhakikisha mawasiliano katika eneo hilo yanarejea.

Naye Mhandisi wa TARURA Wilaya ya Ilala, Magori ameahidi kusimamia usiku na mchana ujenzi wa daraja hilo ili wananchi, na watumiaji wengine waendelee kupata huduma muhimu ya mawasiliano.
Pamoja na kutoa wito kwa madereva wa magari makubwa kutopitisha magari na mizigo yasiyoendana na uzito wa daraja la Magore.
More Stories
Wasira :Tumeshafanya mabadiliko ya sheria za uchaguzi,Chadema hawawezi zuia uchaguzi
Msichana Initiative,PWC wasisistiza umuhimu wa pedi bure kwa wasichanaÂ
Maagizo matano yatolewa kuongeza ufanisi kampuni ambazo serikali ina hisa chache