Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online, Dar
MKUU wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amemsimamisha kazi Mwenyekiti wa Mtaa wa Kinyamwezi, uliopo Kata ya Pugu Jiji Dar es Salaam, Kassimu Mfinanga, kupisha uchunguzi wa tuhuma za kuhusika kuruhusu uuzaji wa viwanja kiholela kwa mtu zaidi ya mmoja huku akijua vina mgogoro, hali inayopelekea kuongezeka kwa migogoro ya ardhi.
Mpogolo ametoa uamuzi huo Januari 26, mwaka wakati wa ziara yake ya kutatua kero za wananchi wa Kata hiyo, ambapo ilibainika kuwepo kwa mgogoro wa ardhi katika eneo hilo kati ya watu watatu na mlalamikaji, ambao kesi yao bado ipo mahakamani.
Mpogolo amemtaka Mwenyekiti huyo wa Mtaa kutojihusisha na shughuli zozote za kiutendaji katika mtaa huo na kusema kuwa, nafasi hiyo itashikiliwa na mtu mwingine mpaka uchunguzi utakapo kamilika.
Pia Mpogolo amewataka watu wote waliopo katika eneo hilo lenye mgogoro kuendelea kuwa watulivu na kutii amri ya Mahakama inayowataka kutoendelea na shughuli za uendelezaji wa eneo hilo ikiwemo ujenzi hadi kukamilika kwa kesi hiyo.
” Tumekuwa tukipata malalamiko mengi kutoka kwa wananchi katika baadhi ya maeneo,kumbe ni kutokana na baadhi ya ubovu wa viongozi wetu, Serikali ya Mtaa inawapa watu maeneo yenye migogoro……..,Mtendaji naomba uwaandikie barua itayoambatanishwa na zuio hili la Mahakama ili watu hawa wasiendelee na shughuli za uendelezaji katika eneo hili,”ameeleza Mpogolo na kuongeza kuwa
“Ni vyema mkatulia amri ya Mahakama hata pale kesi itapoamuliwa kama utakuwa umeshindwa basi utaendelea na kama utakuwa umeshindwa basi utajua nini inatakiwa kufanya lakini kufanya kinyume na kuendelea kujenga alafu baadae unaposhindwa kesi unabomolewa nyuma mnakuja kulalamika Serikali haitusaidii,serikali tumekuja tunawaambia msitishe shughuli za uendelezaji kama Mahakama ilivyoamua Hadi kesi itakapo isha”, amesema Mpogolo.
More Stories
Serikali ya Kijiji Ilungu yawakatia bima za afya wananchi 1500
TMA kuendelea kufuatilia mifumo yake
Wassira:Waliopora ardhi za vijiji warudishe kwa wananchi