November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

DC Mpogolo amshuru Rais Dkt Samia kwa kuwapa bilioni 3.5 za maendeleo

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Mkuu wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan, katika utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi miaka mitatu ya uongozi wake Rais ametoa shilingi bilioni 3.5 za miradi ya maendeleo wilaya ya Ilala.

Mkuu wa wilaya Edward Mpogolo, alisema hayo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Gongolamboto wakati wa kuzungumza na wananchi wa Majohe,Pugu ,Pugu Stesheni na Gongolamboto ambapo alikuwa akipokea kero za wananchi na kuelezea mikakati ya Serikali na mafanikio yake.

“Tunamshukuru Rais wetu mpendwa Dkt.Samia Suluhu Hassan ,katika miaka mitatu ya uongozi wake wilaya yetu ya Ilala ametupatia bilioni 3.5 za miradi ya maendeleo ikiwemo sekta ya afya sekta ya Elimu na Miundombinu ya Barabara ikiwemo masoko “alisema Mpogolo.

Mkuu wa wilaya Edward Mpogolo alisema sekta ya Elimu msingi Rais alitoa shilingi bilioni 18.ambapo Ilala wamejenga madarasa 437 shule mpya 12 ikiwemo kata ya Mnyamani iliyojengwa kwa milioni 300 ambapo kwa sasa imeanza kutoa huduma wanafunzi 600 .

Aidha alisema elimu sekondari Ilala wamepokea bilioni 28 ambapo pesa hizo wamejenga madarasa mapya 645 ambapo madarasa mapya 645 madarasa 80 ya shule za Gholofa ikiwemo Ukonga sekondari ya Gholofa na vyoo tundu 45 sekondari nyingine ya golofa imejengwa Liwiti na Mnazi Mmoja.

Akizungumzia sekta ya maji kata ya Gongolamboto, Pugu ,Pugu Station, Majohe na Kitunda tanki kubwa la DAWASA linaenda sambaza maji la shilingi bilioni 36 na kuwawezesha wananchi wa maeneo hayo kufurahia matunda ya Serikali yao ya Dkt.Samia Suluhu Hassan .

Akizungumzia sekta ya afya Serikali imetoa pesa nyingi sekta ya afya imejenga vituo vingi vya afya katika wilaya ya Ilala na Chanika inatarajia kuwa Hospitali kamili hivi karibuni inapandiishwa hadhi.

Akizungumzia miundombinu ya Barabara alisema Serikali inatarajia kujenga Barabara za kisasa mradi wa kuboresha miundombinu ya jiji DMDP Kilometa 57 wilaya ya Ilala ambapo alisema barabara nyingi zitajengwa.