Na Heri Shaaban, Timesmajira Online -Dar
Dirisha la mkopo wa asilimia 10 inayotolewa kwa makundi maalumu ikiwemo wanawake asilimia nne,vijana asilimia nne na watu wenye ulemavu asilimia mbili,limefunguliwa kwa Halmashauri ya Jiji la Dar-es-Salaam wilayani Ilala mkoani Dar-es-Salaam.
MKUU wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, amefungua rasmi dirisha la mikopo hiyo kwa vikundi 945, huku vikundi mbalimbali vikikabidhiwa hundi.
Amesema,Halmashauri hiyo imetenga zaidi ya bilioni 18, kwa ajili ya kutoa mikopo hiyo kwa vikundi hivyo wilayani humo.
“Utoaji wa mikopo hii ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan,la utoaji mikopo kupitia mfumo jumuishi kwa makundi maalum ,ambao unalenga kuwawezesha wananchi kiuchumi na kuongeza mapato ya halmashauri ” amesema Mpogolo.
Pia,amezitaka taasisi za benki nchini zilizopewa jukumu hilo kutafakari dhamira ya Rais za kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa kutoa huduma sahihi kwa malengo yaliokusudiwa
Akizungumzia changamoto kadhaa ikiwemo ukosefu wa elimu kuhusiana na matumizi ya mikopo,huku dhamira ya Serikali kupitia Halmashauri hiyo ni kuhakikisha kila mnufaika anapata mkopo kulingana na aina ya biashara yake.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji hilo Elihuruma Maberya,amesema,
Mkurugenzi Elihuruma Maberya alisema mpango huo ni jitihada za Serikali za kukuza uchumi kwa wananchi wake, waweze kujikwamua na kukuza mitaji yao.

More Stories
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi
Kihongosi:Uhai wa chama mashina
Kihongosi: Msigombane kwa itikadi za vyama