December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

DC Mayeka: Kamateni mawakala wa mitandao ya simu wanaotoza fedha wananchi wakati wa kuweka

Na Esther Macha, Timesmajira Online, Chunya

SERIKALI wilayani Chunya mkoani mkoani mbeya imepiga marufuku mawakala
wa mitandao ya simu wanaotoza fedha kwa wananchi wakati wa kuweka
fedha kwenye simu zao .

Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya chunya , Mayeka Saimon
Mayeka wakati wa kikao cha baraza la madiwani na kuibuka malalamiko
kwa baadhi ya madiwani kuhusu wananchi kutozwa fedha na wakala wa
mitandao ya simu katika maeneo mbali mbali ya wilaya hiyo.

‘’Lengo letu hapa watu wa mitandao waitwe wajibu hili huu ni wizi
haukubariki hata kidogo ikiwezekana wachukuliwe hatua , kuweka fedha
ni bure ila kwenye kutoa fedha unakatwa kwenye mtandao lakini una
shilingi 100,000 toa 2000 nikuwekee ule ni wizi kama wizi mwingine
niwaombe sana ndugu zangu waheshimiwa Madiwani tusaidiane hili jambo
la wizi tuanze ukamataji wa jambo hili huu ni wizi, kupitia baraza
hili napiga marufuku na yeyote atakapatikana atachukuliwa hatua
,kamateni mawaka wachache wanaotoza fedha wananchi wakati wa kuweka
hii itakuwa fundisho’’amesema Mkuu huyo wa Wilaya.

‘’Mkuu wa polisi wilaya kwa kushirikiana na polisi kata kuanzia leo anzeni msako kukamata
mawakala wote wanaotoza fedha wananchi wakati wa kuweka kwenye simu
zao na kutuma kwani huo ni wizi kama ulivyo wizi mwingine’’amesema

Bosco mwanginde ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya chunya na
Diwani wa kata Mbughani amesema mawakala hao wanaofanya wizi wapo na
sio wa kuwatafuta wapo ni kuwachukua tu na hatua kuchukuliwa ili iwe
fundisho kwa wengine .

‘’Mimi shughuli zangu nyingi nafanyanyia Kata ya Sangambi kule ndiko
mimi nilipata changamoto mara nyingi nikitaka kutuma hela nyumbani
bila shilingi 10,000 unatakiwa kuchangia 500 kwa maana hiyo kama una
hela nyingi unatakiwa kuchangia 500 hawa mawakala wakamatwe maana
kuna kipindi Meneja aliyekuwepo aliwaita na kuwakemea na tabia hiyo
ikaachwa lakini imerudi tena hata wananchi nao naona wamezoea na
kuona ni hali ya kawaida ,nimekuwa nikipokea malalamiko kwa wananchi
ambao ni wanufaika wa TASAF kuwa mbona wanakatwa fedha zao ‘’amesema .

Mkuu wa wilaya ya Chunya
Mwenyekiti halmashauri ya wilaya ya Chunya
Baadhi ya madiwani wa halmashauri hiyo wakiwa kwenye kikao