December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

DC Massala: Wananchi tumueni fursa za kiuchumi stendi mpya Nyamhongolo

Judith Ferdinand,TimesMajira Online, Mwanza

Mkuu wa,Wilaya ya Ilemela Hassan Massala,ametoa wito kwa wananchi kuutunza na kutumia fursa za kiuchumi zinazotokana na uwepo wa mradi wa kisasa wa stendi mpya ya mabasi na maegesho ya malori Nyamhongolo, uliopo wilayani Ilemela mkoani Mwanza.

Huku akitoa pongezi kwa Mbunge wa Jimbo la Ilemela,Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula kwa ushirikiano wake katika kuhakikisha mradi huo unakamilika

Masalla amezungumza hayo mara baada ya kumaliza kwa mbio za Kilomita 8 zilizoanzia Buzuruga Plaza na kufikia tanati katika stendi hiyo za Ilemela maarufu Ilemela Jogging Clubs zinazojumuisha vilabu mbalimbali vya mbio vilivyopo mkoani Mwanza na wananchi wengine.

Amesema,amesema jumla ya kiasi cha fedha bilioni 26.6 zimetumika kukamilisha mradi wa kisasa wa stendi ya mabasi na malori Nyamhongolo.

Hivyo amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwaajili ya utekelezaji wa mradi huo huku akitoa wito kwa wananchi kuutunza na kutumia fursa za kiuchumi zinazotokana na uwepo wa mradi huo ikiwemo vizimba vya biashara.

“Niwaombe wananchi tujitokeze kutumia fursa zitakazopatikana katika mradi huu mkubwa wa stendi ya kisasa Afrika Mashariki inayopatikana Wilaya ya Ilemela ambao umetumia takribani biilioni 26.6 kukamilisha kwake,”amesema Massala.

Mtaalam kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Ahmed Sakibu ameeleza kuwa matangazo kwa ajili ya wananchi kujitokeza kuanza kuomba vizimba vya biashara na maduka makubwa ya kisasa yataanza kutolewa kuanzia siku ya Jumatatu kupitia vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii.

Hivyo amewahimiza wananchi kujitokeza kuomba fursa mbalimbali za kiuchumi zitakazopatikana sanjari kuutembelea mradi huo wakati wowote kabla ya kuanza kutumika rasmi.

Kwa upande wake mmoja ya wananchi waliojitokeza katika kushiriki mbio za Kilomita nane zilizoanzia Buzuruga na kuishia Nyamhongolo stendi Fadhili Ramadhani amempongeza Mkuu wa wilaya ya Ilemela kwa ubunifu wake wa kuanzisha na kuhamasisha mbio hizo.

Kwani mbali na kusaidia katika kupambana na magonjwa lakini pia zimeanza kutumika kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi na kuhakikisha wananchi wanashirikishwa katika kutambua fursa za kibiashara na uchumi

Haya hivyo Wilaya ya Ilemela inaendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati ikiwemo ya sekta ya afya, elimu, miundombinu ya barabara, maji na huduma nyengine za kijamii.

Mkuu wa,Wilaya ya Ilemela Hassan Massala,akizungumza na washiriki pamoja na wananchi mara baada ya kumaliza kwa mbio za Kilomita 8 zilizoanzia Buzuruga Plaza na kufikia tamati katika stendi mpya ya mabasi Nyamhongolo za Ilemela maarufu Ilemela Jogging Clubs zinazojumuisha vilabu mbalimbali vya mbio vilivyopo mkoani Mwanza na wananchi wengine,ambapo ametoa wito kwa wananchi kuchangamkia fursa za kiuchumi zinazopatikana katika stendi hiyo.picha na Judith Ferdinand
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Massala( alievaa fulana ya blue na kofia nyeusi) akikimbia pamoja na washiriki wengine mbio za Kilomita 8 zilizoanzia Buzuruga Plaza na kufikia tamati katika stendi mpya ya mabasi Nyamhongolo za Ilemela maarufu Ilemela Jogging Clubs zinazojumuisha vilabu mbalimbali vya mbio vilivyopo mkoani Mwanza na wananchi wengine.picha na Judith Ferdinand