December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

DC Ludigija aiagiza Ilala kuanzisha Kampuni maalum ya kukamata wachafuzi wa mazingira

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

MKUU wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ludigija ametoa agizo kwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam waunde kampuni Maalum kwa ajili ya kusimamia WACHAFUZI wa Mazingira katika ya Wilaya ya Ilala.

Mkuu wa Wilaya llala Ludigija ametoa agizo hilo katika kampeni endelevu ya USAFI Wilaya ya Ilala Leo Mtaa wa Kongo Kariakoo sambamba na kuwapanga Wamachinga katika utaratibu Maalum.

“Mkuu wa mkoa Dar es Salaam Amos Makala, alizindua kampeni ya usafi mkoa Dar es Salaam leo ni mwendelezo wa kampeni hiyo hivyo tunawataka wananchi wafanye usafi wenyewe bila kusurutishwa na Serikali wale Wananchi watakaoshindwa kufanya usafi wakamatwe iwepo Kampuni Maalum Wakala kwa ajili ya kusimamia swala hili kwa watu wasio fanya usafi”alisema Ludigija.

Ludigija alisema Kampuni Maalum ikianzishwa itakuwa inasimamia swala ziima la usafi katika Wilaya yetu ya Ilala Ili iwe Wilaya Bora katika usafi Ilala

Ludigija aliwataka Maafisa Afya na Maafisa Mazingira kusimamia usafi kila wakati sambamba na utoaji elimu kwa Wananchi na kuweka vifaa Maalum vya Usafi.

Aliwataka Wataalam wa MAZINGIRA na Mipango Miji kushirikiana kufanya ziara katikati ya mji huo kuwachukulia watu wanaweka maji taka sehemu si rasmi.

Katika hatua nyingine Ludigija alisema atafanya ziara Maalum kufatilia ut ekelezaji wa maagizo yake kama yamefanyiwa kazi na wataalam wa Idara ya Mipango Miji na Mazingira .

Wakati huo huo Ludigija aliwataka Maafisa Biashara kuwapanga upya wamachinga wa Mtaa Kongo Kariakoo kwa meza Maalum zinazotambulika na Halmashauri ya la Dar es Salaam.

Kwa upande wake Afisa Mazingira Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam RAJABU NGODA alisema maagizo yaliotolewa na Mkuu wa Wilaya watayatekekeza katika suala zima la kuakikisha Ilala inakuwa safi.

Ngoda aliwataka wananchi kutupa taka Katika maeneo Maalum yaliotengwa ikiwemo vifaa vya kuifadhia taka.

Kiongozi wa Machinga KARIAKOO Yuduph Namoto alisema wataunda KAMATI Maalum kusaidia Serikali katika suala la usafi .