November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

DC Kilombero apiga marufuku ufugaji, kilimo kando ya mto

Na David John, Timesmajira Online Kilombero

SERIKALI ya Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro imetoa maagizo matatu Kwa wananchi wa Wilaya hiyo kuacha mara moja kufanya shughuli za Kilimo, ufugaji, pamoja na ukataji wa miti na a mefunga vibari vyote vya kukata miti kwa lengo la kutunza na kuhifadhi vyanzo vya Maji pamoja na mazingira kwneye Bonde la mto Kilombero.

Pia imesema kuwa Bonde la Kilombero linachangia asilimia 65 ya Maji katika Bwawa la Julius Nyerere hivyo wao kama Wilaya Wanawajibu mkubwa na umuhimu wa kulinda na kuhifadhi vyanzo vya Maji katika Bonde hilo .

Akizungumza mbele na waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya Habari ofisini kwake wilayani humo ambao walikuwa wameongozana na watalamu kutoka Bodi ya Maji Bonde la Rufiji Iringa Mkuu wa Wilaya Dunstun Kyobya amesema nimarufuku kuazia Sasa kuona ufugaji,kilimo na shughuli zingine za kibinadamu pembezoni mwa Bonde la mto Kilombero .

“Hapa ninavyozungumza tumeshakamata Ng’ombe 201 na tumewafikisha Mahakamani na Mahakama wamezitaifisha na wamekata Ng’ombe zingine 148 nazo kesi yake Iko Mahakamani .”amesema

Nakuongeza kuwa ” Namshukuru sana Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan,Waziri wa Maji Jumaa Awesu na Bodi ya Maji Bonde la rufiji Kwa kuweza kusisitiza umuhimu wa utunzaji wa vyanzo vya Maji ,lakini kipekee nimshukuru Rais. Samia Kwa kuweza kutoa Goverment Notes (GN) ya kutambua mipaka katika Bonde la Kilombero.”amesisitiza

Pia Mkuu wa Wilaya Kyobya amesema anawatia moyo sana Bodi ya Maji Bonde la Rufiji Kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya na wao Kama Wilaya watahakikisha wako pamoja nao ili kuhakikisha kwamba Mabonde yote yanakuwa salama Kwa maana Bonde la Kilombero na Bonde la Ruaha.

Akizungumzia zaidi umuhimu wa kutunza vyanzo vya Maji amesema wilaya yake inakutana na wafugaji waliopo ndani ya Wilaya hiyo ili kuweza kupeana utaratibu lakini pia kuona njia njia na namna nzuri ya wao kuweza kuondoka pasipo kuasili vyanzo vya maji na mashamba ya wakulima katika njia watakazo kuwa wanapita.

Wakati huo huo mkuu wa Wilaya amezungumzia utekelezaji wa miradi mbalimbali kwenye sekta ya miundombinu ya barabara ,shule,pamoja na vituo vya afya,Hospitali na huku akimshukuru Dkt Samia Kwa kuendelea kuongeza watumishi katika kila Taasisi ya Serikali.

Kwa upande wake mhandisi Emmanuel Lawi ambaye ni Afisa Maji kidakio cha Mto Kilombero amesema kuwa mto huo Kwa juu unapitisha Maji Kwa ujazo wa Bilioni 19 Kwa mwaka ambayo ni mchango kwa Bwawa la mwalimu Nyerere Kwa asilimia 65.

Amefafanua kuwa kulikuwa na changamoto kubwa kutokana na uwepo wa shughuli za kibinadamu kama kilimo mifugo na lakini Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amepandisha hadhi kwenye Bonde hilo Kwa kuweka GN lakini pia Mkuu wa Wilaya hiyo amekuwa akipambana kuhakikisha kuwa vyanzo vya Maji vinalindwa.

Ameongeza kuwa mto huo ulikuwa umeharibika lakini Mkuu wa Wilaya hiyo Dunstun Kyobya amekuwa balozi mzuri wa mazingira na wao kama watalaamu wataendelea kushirikiana Kwa ajili ya kuhakikisha vyanzo vyote vya Maji vinalindwa .

Naye mwananchi wa eneo hilo Mohamed Mnanjale. Ameiomba Serikali kuwaondoa wafugaji na wakulima katika eneo la Bonde la Mto Kilombero kwasababu Ng”ombe wanaharibu sana vyanzo vya Maji na na uharibifu mkubwa wa mazingira .