January 19, 2022

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

DC jokate kuwania tuzo za kidigitali Tanzania,2021

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo amechaguliwa kuwania tuzo za kidigitali Tanzania, 2021 kwenye vipengele vinne vya tuzo hizo.

Vipengele vya tuzo hizo ni;

1. Kiongozi bora wa Serikali (Mwanamke) kwenye mitandao ya kijamii

2.Mwanasiasa bora wa kidigitali

3.Mshawishi bora wa mwaka

4.Chaguo bora la watu

Pia Mkuu huyo wa Wilaya amesema mitandao ya kijamii imemsaidia kwenye vitu mbalimbali ikiwemo kufikisha ujumbe kwenye jamii;

“Binafsi mitandao hii imenisaidia sana kufikisha ujumbe na kupata ‘support’ (Ushirikiano) ya watu wengi katika kufanikisha malengo na shabaha za serikali sambamba na malengo binafsi ninayojiwekea kama kiongozi katika kuchagiza yale makubwa ya serikali kwenye nafasi ya uongozi niliyoteuliwa kutumikia”

Aidha Dc Jokate amewashukuru wote kwa kuonesha ushirikiano kwenye tuzo hizo;

“Nitumie fursa hii adhimu kushukuru sana wote walionipendekeza kuwania kwenye vipengele vinne vya tuzo hizi, pia nawapongeza sana waandaaji wa Tuzo hizi” Amesema Dc Jokate