November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

DC JOKATE: kuja na mkakati wa kukomesha uhalifu nje ya uwanja wa Mkapa

Na Mwandishi wetu,TimesMajira,Online

Mkuu wa Wilaya ya TemekeĀ  Jokate Mwegelo ameweka wazi mbele ya waandishi wa habari dhamira yake ya kubadilisha taswira ya muonekano wa eneo la mbele la ofisi yake iliyopo uwanja wa Benjamin Mkapa Temeke, Dar es Salaam.

Akiongea katika eneo la tukio mapema leo Mkuu wa Wilaya amesema eneo hilo lina taswira ya Kitaifa na Kimataifa kwa kuwa  hutumika katika michezo na dhifa mbalimbali.

Pia eneo hilo ndipo ilipo ofisi ya Mkuu wa Wilaya ambalo nyakati za usiku huwa na giza linalopelekea vitendo vya kihalifu kufanyika.

“Mkuu wa Wilaya ni mwenyekiti wa ulinzi na usalama haitaleta afya hata kidogo uhalifu kufanyika eneo la ofisi ya Mkuu wa Wilaya na kwa Temeke usalama ni moja ya kipaumbele” AmesemaĀ  Mwegelo.

Kwa upande wa Meneja wa TARURA ambaye pia ni mratibu wa uendelezaji  Jiji la Dar es Salaam  amesema kuwa zoezi hilo la ukarabati na uwekaji wa taa 32 katika eneo hilo la barabara lenye urefu wa kilometa 1.3 litagharimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 102 na litakamilika baada ya majuma mawili mara baada ya taratibu nyingine kukamilika.

Aidha Diwani wa kata ya Miburani Juma Mkenga amemshukuru Mkuu wa wilaya kwa kutambua umuhimu wa eneo hilo na kwamba uwekaji wa taa hizo kwa kiasi kikubwa utapunguza matukio ya uhalifu.

Eneo hilo kwa kipindi kirefu limekuwa likilalamikiwa na wananchi kwa kukithiri kwa vitendo vya kiuhalifu kama uporaji hasa nyakati za usiku.