Na Mary Margwe, TimesMajira Online, Busega
Mkuu wa Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu Anna Gidarya amekabidhi sare za Shule, madaftari 9 kwa kila wanafunzi 38 wa Kidato cha kwanza shule ya Sekondari Venance Mabeyo iliyopo Kata ya Kabita Wilayani humo.
Akikabidhi sare za Shule pamoja na madaftari kwa wanafunzi hao Mkuu huyo aliwataka wanafunzi hao kuhakikisha wanazitunza sare hizo pamoja na hayo madaftari waliyokabidhiwa ili kuweza kuwatia Moyo walijitolea.
Gidarya alisema Serikali ya awamu ya sita chini ya mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeweka Miundombinu dhabiti kwa shule Kwa kujenga Madarasa, kuweka Madawati ili wanafunzi wasome bila kutoa visingizio visivyo vya lazima, hivyo ni wakati mzuri wa wanafunzi kumrudishia Rais Dkt.Samia fadhila za kusoma kwa bidii zaidi na hatimaye kuweza kufikia malengo mliyojiwekea.
” Kikubwa hakikisheni mnaongeza bidii katika masomo, huu ndio muda wenu sasa wa kujihakikishia hatma ya maisha yenu, maisha yanaandaliwa hapa, hivyo some I Kwa bidii na kwa malengo mliyojiwekea” alisema Gidarya
Wakiongea Kwa nyakati tofauti wanafunzi hao walioshukuru Kwa kupatiwa msaada huo ambao wameuchukulia kama ni Mungu tu amewapelekea sare za Shule pamoja na madaftari 9 kwa kila mmoja Kwa wanafunzi hao 38.
” Tunamshukuru Mungu hakika hatukua tumetarajia kabisa kama sisi leo tungepata huu msaada, lakini kwakua kwa Mungu hakuna kinachoshindikana kwa mungu, hivyo tunaamini na hili ni Baraka zake” alisema mmoja wa wanafunzi waliopata msaada huo.
More Stories
Simbachawene:Waombaji wa ajira jiungeni na Mfumo wa Ajira Portal
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki