January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

DC.Bunda ahimiza wazazi kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula shuleni

Na Raphael Okello Bunda.

MKUU wa Wilaya ya Bunda Dkt. Vicent Naano amewataka wazazi na walezi wilayani Bunda kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula shuleni ikiwa ni hatua ya kuboresha elimu wilayani humo.

Akizungumza na Wananchi wa Mtaa wa Kiwasi katika mkutano uliofanyika shule ya msingi Kiwasi Dkt. Naano amesema suala la chakula shuleni ni maelekezo ya Serikali kwamba wanafunzi wote shuleni wapate chakula.

Ambapo pia ameiagiza Serikali ya Mtaa kusimamia zoezi hilo ili wazazi au walezi waweze kuchangia chakula cha watoto wao shuleni.

Amesema endapo mzazi,mlezi atakaidi kuchangia basi achukuliwe hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kutozwa faini ambayo itasaidia shughuli za maendeleo katika shule hiyo.

Pamoja na suala la chakula shuleni Dkt . Naano pia amewataka wananchi wa Mtaa wa Kiwasi kuacha kubweteka badala yake wakarabati shule ya msingi Kiwasi iliyojengwa tangu mwaka 1975.

“Shule hii yenye majengo ambayo yameanza kuchoka inahitaji angalau madarasa mawili kila mwaka ambapo Serikali itawaunga mkono mbele ya safari,”ameeleza.

MKUU hiyo wa Wilaya ya Bunda amekabidhi jukumu hilo kwa Serikali ya Mtaa kuhakikisha inaandaa utaratibu mzuri utakao kuwa rafiki kwa watu wote kushiriki.

Hata hivyo baadhi ya wananchi wamedai kuwa serikali imekuwa ikihamasisha chakula shuleni lakini imekuwa ikishindikana na kwamba inahitajika elimu ya kutosha Ili wazazi wote wajue umuhimu