December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

DAWASA yafungua dawati la huduma kwa wateja

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imefungua dawati la huduma kwa wateja kwa ajili ya kutoa elimu kwa umma juu ya huduma mbalimbali za Mamlaka ikiwemo utaratibu wa upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi wa Kata ya Majohe, Wilaya ya Ilala ambao ni sehemu ya wanufaika wa utekelezaji wa mradi wa maji Majohe.

Utekelezaji wa mradi wa maji Majohe umehusisha ulazaji wa mabomba ya inchi 8,6,4 na 3 kwa umbali wa kilomita 46 na utahudumia wananchi takriban 24,000.