LUSAKA, Zambia
ALIYEKUWA mshambuliaji wa klabu ya Yanga, David Molinga amekamilisha usajili wake wa kujiunga na miamba ya soka nchini Zambia, klabu ya ZESCO United kwa ajili kuitumiki kwenye Ligi Kuu msimu huu nchini humo.
Molinga raia wa DRC Congo aliitumikia klabu ya Yanga kwa muda wa mwaka mmoja huku akiwa mfungaji bora wa klabu hiyo katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita.
Hata hivyo, klabu ya ZESCO, inasuka upya kikosi chao na muda mfupi uliopita wamemfuta kazi ya Ukocha Mkuu, George Lwandamina, ambaye licha ya kutwaa Ubingwa wa ligi mara mbili, lakini msimu uliopita ulikuwa mbovu kwenye Historia ya klabu hiyo takribani miaka Tisa.
Mbali na hivyo pia klabu hiyo imekosa Ubingwa na hawatoshiriki Michuano ya vilabu Afrika. Huku wakishika nafasi ya tano katika Ligi Kuu Zambia msimu uliopita.
%%%%%%%%%%%%%%
More Stories
Naibu Waziri wa Fedha abariki ujio mpya wa Bahati Nasibu
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes