Na Heri Shaaban , TimesMajira Online, Ilala
KATIBU Tawala wa wilaya ya Ilala Charangwa Selemani , amewataka wanawake wa Tabata KIMANGA, kujikwamua kiuchumi waache kuwa tegemezi ili waweze kufikia malengo yao katika kuisaidia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kukuza uchumi.
Katibu Tawala Charangwa Selemani ,ameyasema hayo kata ya Kimanga wakati wa uzinduzi wa jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi ambapo kila kata ndani ya wilaya Ilala majukwaa ya wanawake yanazinduliwa kwa ajili ya kuwaunganisha wanawake waweze kupata fursa mbali mbali za serikali katika vikundi vyao.
“Mimi ni mwanamke mwenezu nawahasa wanawake wezangu wa Tabata KIMANGA msilale muamke mjikwamue kiuchumi katika majukwaa yenu mjenge umoja na mshikamano muweze kuchangamkia fursa za kiuchumi mkitoka biashara zenu zitatoka na mkilala na biashara zenu zinalala”amesema Charangwa
Katika uzinduzi huo wa Jukwaa la wanawake KIMANGA Katibu Tawala Charangwa amewatuniisha mfuko wa jukwaa hilo kwa harambee ya Keki ambapo viongozi mbalimbali na wadau walichangia keki hiyo akiwemo Katibu Tawala Charangwa akitoa shilingi 100,000 /=GRACE ZOA ZOA shilingi 100,000/= KMJ hospitali ya Tabata Kimanga shilingi 100,000 /= AKha Khan shilingi 60 000/= Diwani Pastory Kyombiya 100,000/=na Jukwaa la Wilaya ya Ilala shilingi 50,000/=
Katibu Tawala Charangwa amewataka Wanawake wapendane wasaidiane na kupeana fursa kwani wanawake wanaweza hivyo wapewe fursa na kupeana moyo na kuwa wabunifu katika kutengeza bidhaa mbalimbali.
“Majukwaa ya uwezeshaji wananchi kiuchumi yalianzishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan wakati akiwa Makamu wa Rais wa Tanzania kwa lengo la kuwaweka wanawake pamoja na ili wapeane fursa “amesema.
Diwani wa Viti Maalum wilaya ya Ilala RUKIA MWENGE amewataka Wazazi kulea watoto katika misingi mema na kuwataka wanawake kujenga mtandao wa Biashara yoyote ina pesa wakifanya watanyanyuka mitaji yao na kukuza uchumi wa nchi yetu .
Aidha pia amewataka wanawake watumie krimu nzuri kwa ajili ya afya yao vipodozi vingine vya kupaka mwilini sio salama kiaya zinaleta madhara kwa Wanawake.
Diwani wa viti Maalum Wanawake Dkt Julieth Banigwa ,amewataka Wanawake kutenga Bajeti kwa ajili ya kukuza mitaji yao ya Biashara na kuwataka Wanawake wa wilaya ya Ilala kujiepusha na mikopo ya kausha damu
Diwani wa kata ya Kimanga Pastory Kyombya, amewapongeza wanawake wa Jukwaa Kimanga kwa uzinduzi wa Jukwaa hilo na kuwataka Wanawake wa Kimanga kuunda vikundi vya ujasiriamali waweze kupata fursa mbalimbali ikiwemo mikopo ya Serikali ya asilimia kumi ambayo inatolewa ngazi ya Halmashauri .
Diwani Pastory Kyombya amesema Wanawake wana uwezo mkubwa katika shughuli za kiuchumi hivyo wajishushulishe na kuunda mtandao wao wa biashara wajenge umoja na mshikamano ili majukwaa yao yaweze kusonga mbele kwani yanatambulika kisheria.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba