Na Mwandishi Wetu,TimesMajira
KATIKA kuunga jitihada za wajasiriaamali wasusi,kampuni inayoongoza katika bidhaa za nywele nchini, Darling Hair imepanga kuhakikisha inawainua na kuwanufaisha wasusi katika mikoa yote Tanzania.
Hatua hiyo inafuatia kampeni maalum ‘ Loyalty Program’ ambayo inalenga kurudisha kwa jamii kwa njia ya kuwapa uwezo zaidi wasusi wadogo wadogo.
Akizungumza katika uzinduzi wa awamu ya pili ya Loyality Program, Meneja Saluni wa Darling Hair Joyce Mwijage alisema, awamu ya kwanza ya programu hiyo ilipata mafanikio makubwa ambapo idadi ya wasusi iliongezeka kutoka 5000 hadi 15,000.
Amesema washiriki walikusanya lebo za bidhaa za Darling Hair na kujizolea pointi kadhaa ambazo ziliwawezesha kujipatia zawadi mbalimbali.
“Lengo la program hii ya Loyalty ni kuwazawadia wasusi wadodo wadogo ili waweze kujiendeleza na hatimaye kufungua saluni zao wenyewe kutokana na vifaa vya saluni wanavyojishindia kwa kukusanya lebo za bidhaa zetu na kujizolea pointi kwa kila lebo.”Amesema.
Ameongeza kuwa baada ya Dar es Salaam.watahamia katika mikoa mingine ambapo amewataka wasusi hao kujipanga kwa kampeni hiyo ambayo kwa mujibu wa meneja huyo, ni ya kudumu.
Shughuli hiyo ya uzinduzi wa awamu ya pili ilifanyika katika Ukumbi wa Sinza Deluxe ambapo wasusi kutoka maeneo mbalimbali walijumuika katika tafrija ya aina yake iliyofadhiliwa na Darling Hair.
Kulikuwa na zawadi, michezo mbalimbali, mziki uliopambwa na wasanii mbalimbali akiwemo msanii maarufu, Click Master ambaye alikonga nyoyo za wasusi hao kwa vibao vyake kama Watajua na Sherehe na kuwaacha wasusi na wawakilishi wa Darling kucheza na kuimba kwa furaha.
Baadhi ya wasusi waliiopongeza kamouni hiyo ya Darling na kusema.kuwa zawadi inazowapa kwa kuumia bidhaa zao inawapa Hamasaki kubwa zaidi katika kazi zao.
Asnath Asajile ambaye ni mmoja ya waliozawadiwa TV na kampuni hiyo.pamoja na kushukuru aliwapongeza kwa kuwathamini katika.kazi za mikono yao.
“Hawa Darling Hair tuwape maua yao.kwa kweli wanatujali sana fikiria kuna mtu alikuwa hana kitu lakini sasa hivi amefanikiwa kumiliki saluni yake chini ya kamoeninya ya Loyalty,”Amesema
Naye Joyce Ngoda amesema kampeni hiyo ni nzuri na inawapa hamasa ya kufanya kazi kwa bidiii zaidi ili kuhakikisha wanajizolea pointi ambazo zitawawezesha kuzawadiwa vitu mbalimbali.
Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na uongozi wa juu kabisa wa Darling Hair ambao waliwapongeza wasusi hao kwa kuendelea kuiamini Darling na bidhaa zake.

More Stories
REA yatoa pole kifo cha Mfalme Harald V
Miss Universe Tanzania, Hexagon zaingia ubia
NMBF yatenga Bill.1 kwa uwezeshaji wa vijana 50