November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Daktari aeleleza wasichokijua wengi kuhusu uwezo wa mbegu za kiume

Na Aveline Kitomary,TimesMajira oneline ,Dar es Salaam

DAKTARI Bingwa wa Wanaume kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila iliyopo jijini Dar es Salaam,David Mgaya amesema sababu mojawapo ya mwanaume kushindwa kusababisha ujauzito ni ubora na uwezo wa mbegu.

Katika mahojiano maalum na Gazeti la  MAJIRA , Dk Mgaya amesema uwezo hutegemea umbo la mbegu na kasi ya kusafiri kufikia yai.

“Mmoja wapo ni shida ya kimaumbile ,uwezo wa mbegu  mwanaume anazozalisha zinaweza kuwa na kiwango kidogo  au mbegu zinashida ya kimaumbile katika  mwonekano wake.

“Mbegu za mwanaume huwa zinagawanyika kuna  kichwa,mwili na  mkia tukizungumza  ulemavu wa mbegu tunazungumzia kuanzia kwenye kichwa  kinakuwa na mwonekano gani? zinakuwa zimechongoka kama yai vile lakini kikiwa cha duara hapo kuna changamoto,kuna mwili na mkia  je ukoje? ni mrefu au mfupi je umegawanyika mara mbili au moja hivi vyote vinazingatiwa.

“Mbegu zingine unakuta ziko na vichwa viwili ,lakini kuna ujazo wa kutosha ,na je mbegu hizo zinaishi na  kama zinaishi ni kwa kiwango gani? Kwasababu zinaweza kutoka nyingi zikiwa zimekufa na haziwezi  kurutubisha,”alieleza Dk Mgaya.

Amesema sababu zingine za mbegu kukosa ubora na uwezo ni  ulevi kupindukia.

“Mbegu zinatakiwa ziwe za kutosha na uwezo wa kusafiri kufata yai kwasababu mbegu zinamuda wa kuishi  zinaweza kufa kama haziwezi kusafiri kwenda kwenye yai zitakufa kabla ya muda.

“zingine kutokana na ulemavu zilizonazo  haziwezi kusafiri kwenda mbele kwasababu zinakuwa zinarudi  kinyume nyume haziendi mbele au mwendo haueleweki hazirudi nyuma au kwenda mbele ,kwahiyo mbegu ikiwa na ulemavu unaweza kushindwa kusababisha ujauzito,”amebainisha.

KIWANGO CHA UBORA KINACHOTAKIWA

Dk Mgaya amesema kiwango cha ubora wa mbengu za kume kinatakiwa kuwa 1.5 mililita kisipungue na kikizidi inatakiwa iwe 7.2 na kiwango cha mbegu mililita ujazo 15 mara 10 kwa sita ,kiwango cha mbegu katika manii inatakiwa isiwe chini 39 mara 10 kwa kipeuo cha sita kwa mkupuo mmoja .

“Uwezo wa mbegu kusafiri inatakiwa kuwa isiwe chini ya asilimi 40 na pia mwendo wa kuelekea mbele usiwe chini ya asilimia 32.

“Umbo la mbegu isipungue asilimia nne mbegu hazihitaji kuonekana zimegandana pia ziwe na mnato chini ya sentimita mbili, mbegu zikizingati uwezo huo tunasema iko katika hali ya kawaida na zinaweza kutunga mimba na kama haziko hizo zinaweza kusababisha kutokutungisha mimba,”alifafanua Dk Mgaya.

Amesema kuwa  korodani kutokuwa katika sehemu yake uzalishaji wa mbegu unaweza kuathiriwa.

ameishauri  wanaume kupata muda wa kuchunguza tatizo na sio kuwashutumu wanawake endapo watashindwa kupata mimba.

“Kama mwanaume  usikimbilie kumuacha mwanamke tafuteni ufumbuzi kwanza  na kudumisha mahusiano bora itakusaidia kuimarisha afya ya kimwili na mahusiano wakati wa tendo la ndoa .

“kwasababu sio suala ya mbegu tu kuna matumizi ya vifaa vya elekroni ,kuna watu wanafanya kazi kwenye viwanda wanakutana na mazingira tofautitofauti ,au pia alipata magonjwa yakamsababishia hiyo hali.

“Wanatakiwa kwenda kupata ushauri wa kitaalamu katika kusikilizwa sababu zinaweza kuwapatia ushauri na pia wataelekezwa na tatizo litatatuliwa.

Mwishoooo….