September 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

CWT Igunga yatoa neno walimu kupandishwa madaraja

Na Lubango Mleka, Timesmajira Online – Igunga

CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT) Wilaya ya Igunga mkoani Tabora kimempongeza na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapandisha madaraja takribani walimu 1058.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa CWT wilayani Igunga, Mwalimu Charles Mganda alipozungumza na Mwandishi wa Habari hii juzi kwenye ofisi za chama hicho ambapo ametoa shukrani hizo kwa niaba ya walimu wilayani hapa.

“Hii ni kwa mchanganuo ufuatao, Walimu wa shule za sekondari ni 261, Walimu wa shule za msingi ni 797,”amesema Mwl. Mganda.

Ametaja faida za kupandishwa madaraja kwa wakati kuwa ni kuongeza morali na nguvu ya kufanya kazi katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

“Kwa kufanya hivyo itachangia ufaulu kuongezeka hata kama hapo kabla waliendelea kufanya kazi kwa umilivu na kupata matokeo mazuri, lakini kupanda kwa madaraja kutawafanya Walimu hawa kuongeza ufaulu zaidi,” amesema Mganda.