January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Curry azidi kuweka rekodi NBA, apiga alama 37 kuiua Sacramento Kings

SAN FRANCISCO, California

NYOTA wa Kikapu katika timu ya Golden State Worriors Stephen Curry, amezidi kuweka rekodi kwenye Ligi Kuu ya Kikapu nchini Marekani NBA, baada ya mwishoni mwa wiki kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa vikapu 117-113 dhidi ya Sacramento Kings.

Katika mchezo huo, Stephen Curry ameifungia timu yake alama 37 na kuweka rekodi ya NBA alama ya tatu kwa mwezi akiwa na alama 85, Green ilikuwa na marudio 14 na 13 katika ushindi wa nne. Hiyo inalingana na safu ndefu zaidi ya ushindi wa timu hiyo msimu huu.

Mara baada ya mchezo huo Curry amesema, siku zote huwa anaumia pindi anapokuwa nje na kuona wenzake wakicheza lakini anapoingia Uwanjani anafanya kile kinachostahili kuhakikisha timu yake inapata matokeo mazuri.

Kufuatia ushindi huo, katika mwezi April Curry amemzidi James Harden kwenye Ligi Kuu ya NBA msimu huu.

Kwa upande wake kocha wa Golden State Worriors Steve Kerr alisema, amemsifia mchezaji wake Stephen Curry kuwa ni mtu mwenye kpaji cha hali ya juu kutokana na uwezo mkubwa anaouonesha msimu huu katika Ligi Kuu ya NBA.

Kwa upande wa Sacramento Kings, nyota a timu hiyo Harrison Barnes ameifungia timu yake alama 23 na marudio saba dhidi ya timu yake ya zamani huku Buddy Hield alifunga alama 25 kuiongoza Kings.