Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MKUU wa Majeshi ya Ulinzi (CDF),Jenerali John Mkunda kupitia Uratibu wa Baraza la Michezo la Majeshi ya Ulinzi Dunia(CSIM),imewaleta Wakufunzi na Wataalum wa masuala ya Ukocha wa mpira wa miguu kutoka nchini Uholanzi kwa lengo la kutoa mafunzo kwa Makocha Wanajeshi na Askari wa nchini Tanzania.
Mafunzo hayo yatatolewa ndani ya wiki mbili kwa lengo la kuwafua makocha hao na kuwa walimu wazuri watakaosaidia timu zao za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) zinazoshiriki ligi mbalimbali nchini na za Taifa.
Dhamira ya CDF ni kuhakikisha kunakuwepo na walimu wazuri watakao saidia timu zao ndani ya Jeshi pamoja na kuongeza mahusiano mazuri kati ya Tanzania na nchi ya Uholanzi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti makocha ambao ni Maafisa wa JWTZ na Askari wamemshukuru CDF kwa kuona umuhimu wa mafunzo hayo kwa makocha na kwamba wakufunzi wa TFF wamekuwa wakitoa mafunzo mbalimbali kwao lakini walimu hao wakigeni wana ujuzi zaidi ambao wataweza kuuongezea.
Walisema watahakikisha ndani ya kipindi cha mafunzo haya watafanya vizuri katika kuhakikisha timu za majeshi na Taifa zinafanya vizuri.
Mafunzo haya ni ya wiki mbili ambapo Septemba 13 mwaka huu yanatarajiwa kufungwa rasmi,mafunzo haya yanatokana na mahusiano mazuri ya Chama Cha Mpira wa miguu Cha majeshi .
More Stories
Mhandisi Samamba awasisitiza maafisa madini kusimamia usalama wa migoni msimu wa mvua
Wapinzani kutimkia CCM ishara ya ushindi Uchaguzi Serikali za Mitaa
Vikundi Ileje vyakabidhiwa mikopo ya asilimia 10, DC Mgomi avipa somo