May 15, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

CRDB yatarajia kutoa gawio la Tsh.65 kwa kila hisa

Na Queen Lema, Timesmajira Online,Arusha

Benki ya CRDB,imefanikiwa kupata faida ya bilioni 551 ambapo wanahisa wake watarajiwa kupitisha na kisha kunufaika na gawio la Tsh.65 kwa kila hisa,kupitia mkutano wa 30 wa benki hiyo.

Akiongea na vyombo vya habari jijini Arusha Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya CRDB,Dkt. Ally Laay,amesema kwa kipindi cha mwaka huu benki hiyo imefanikiwa kufanya vyema.

Ambapo amefafanua kuwa gawio kwa kila hisa litakuwa shilingi 65 tofauti na awali ambapo gawio lilikuwa shilingi 50.

Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo,Abdulmajid Nsekela,amesema kuwa, mpaka sasa thamani ya benki hiyo ni tirioni 17.6 huku faida ikizidi kuongezeka.

Nsekela amesema,benki hiyo imepanua wigo mpaka nje ya nchi ambapo kwa sasa wapo kwenye nchi ya Burundi,Congo, huku mikakati ni kufika Dubai.