March 1, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

CPA.Makalla atembelea miradi ya kimkakati kusini Pemba

Na Agnes Alcardo,TimesmajiraOnline

KATIBU wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa CPA. Amos Makalla, leo tarehe 27 Januari 2025 ameendelea na ziara yake ikiwa ni siku ya pili Visiwani Pemba ambapo leo alikuwa Kusini Pemba .

Makalla akiwa kusini Pemba amefanya ukaguzi wa Miradi ya kimkakati akianzia Shule ya Kisasa na ya Mfano ya Sekondari ya Ole iliyopo jimbo la Chake Chake ya Ghorofa tatu yenye Madarasa 40, kisha akakagua Mradi wa Mkubwa wa Maji wa Kendwa uliogharimu Bil 40 ambao upo jimbo la kiwani pamoja na mradi wa Hospital ya Rufaa ya  Abdallah Mzee, akimalizia kukagua mradi wa Bandari uliopo katika Jimbo la Mkoani Kusini Pemba.

Makalla, amesema wajumbe wa Mkutano Mkuu waliona mbali na kuamua kuwateua wagombea mapema, ili kuendeleza kazi nzuri walioifanya kwani mambo yanayofanyika Zanzibar hayahitaji tochi kuyaona kila sehemu imebadilika, lazima tuwapongeze kwa kazi nzuri dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na Dkt Hussein Mwinyi kwa kutekeleza Ilani kwa vitendo.