BEIJING,
Serikali ya China inasema kuna wagonjwa wapya 31 wa ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) na vifo vinne. Hayo ni kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa jana na Kamisheni ya Afya ya nchi hiyo.
Miongoni mwa wagonjwa hao 31, walitoka nje ya nchi hiyo, na ni mmoja tu aliyeambukizwa katika Jimbo la Kaskazini Magharibi la Gansu. Wagonjwa wanne waliofariki dunia ni kwenye jimbo la Hubei, chimbuko la maambukizi ya kirusi cha corona, ambalo hata hivyo halina mgonjwa mpya.
Jimbo hilo lililokuwa kwenye marufuku ya kutotoka nje, limeanza kurejea kwenye maisha yake ya kawaida. Maambukizi kutoka nje ndicho kikwazo kikubwa kwa China kwa sasa, baada ya juzi Baraza lake la Taifa kutangaza kwamba kimsingi nchi hiyo imefanikiwa kuuzuwia ugonjwa wa COVID-19.
Tangu kirusi hicho kianze kusambaa mwezi Desemba mwaka jana, watu 81,470 wameambukizwa nchini China pekee, ambako 3,304 wamepoteza maisha.
More Stories
Dk. Mpango amwakilisha Samia sherehe za Uhuru wa Lesotho
Samia atangaza Tanzania kumuunga mkono Odinga
Tanzania yaongoza kikao maalum cha nishati safi