NAHODHA wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya Aston Villa inayoshiriki Ligi Kuu England Mbwana Samatta, ni miongoni mwa watu wenye simanzi kubwa wakati huu wa janga la virusi vya corona (Covid-19) lililoikumba dunia.
Akiweka wazi jambo hilo, Samatta alisema, amekuwa na mawazo sana hasa kuhusu hili janga la Corona kwani huwa anawafikiria sana wale waliopo Magerezani.
“Haya maisha ya kuwa tu ndani yamenifanya niwafikirie zaidi wenzetu waliopo magerezani, nina uhuru wa kwenda supermarket na kula chakula ninachokitaka achana na tv, simu, kitanda chenye joto, wenzetu hawana hivi vitu, tuwaombee sana wanayopitia ni magumu,” alisema Samatta.
Samatta alijiunga na Aston Villa mwaka huu, akisaini mkataba wa miaka minne na nusu akitokea KRC Genk ya Ubelgiji hadi sasa amecheza game 6 na kufunga magoli 2 kabla ya Ligi kusimama.
More Stories
15 wajinoa Juventus,akiwemo mtoto wa Mwenyekiti wa CCM Mbeya
Za Kwetu Fashion Show, yawapaisha wanamitindo nchini
TCAA yaadhimisha siku ya usafiri wa anga Duniani kwa kushiriki mbio za Marathon UDSM